The House of Favourite Newspapers

Magari ya Mondi Yazua Jambo

0

WANANZENGO sio watu wazuri! Wakati ikiaminika ‘yadi’ ya msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ au Mondi imesheheni magari mengi ya kifahari, watu wamemzulia jambo kwamba, eti kuna siri nyuma ya pazia kuhusu kuyamiliki.

 

Mwananzengo mmoja ambaye ameomba hifadhi ya jina lake, amesema msanii huyo huwa anaonesha bosheni magari hayo, lakini mengi si yake, anawatangazia biashara wauzaji wa magari hayo.

“Jamani nyie tuulizeni sisi tunaomfahamu huyo Diamond, sio kila gari analotangaza huwa linakuwa lake.

“Kuna mtu ana yadi kubwa ya magari (anataja jina la huyo mtu), ndiyo huwa mara nyingi anaingia naye makubaliano ya kumtangazia biashara yake hususan yale ma Toyota Land Cruiser V8, huwa anampa magari Mondi ili amtangazie biashara na siyo kwamba ni ya kwake.

 

“Pia kama hamjui, hata zile gari mnazoziona kapaki pale nyumbani kwake Mbezi Beach, ni za huyo mtu, na yeye ndiye huwa anamtengenezea plate number ziloandikwa kwa jina lake, hata yale aliyomzawadia mama yake na aliyekuwa mchumba wake Tanasha, pia si yake,” alisema mtu huyo.

 

Ili kupata ukweli wa jambo hilo, RISASI JUMAMOSI, lilimtafuta meneja wa matukio na maisha ya wanamuziki wa Wasafi Classic Baby (WCB), Hellen Kazimoto ambaye alikanusha madai hayo kuwa si ya kweli na kusema, watu wanazungumzia ili kumchafua msanii wao.

“Diamond ni msanii mkubwa, inakuwaje akodi magari halafu akayapaki nyumbani kwake au kufanya mambo ya shoo off. Ninachokijua magari anayotembelea ni yake na hata aliyopaki pale nyumbani, pia ni yake. Hizo ni stori zinazungumzwa tu na hazina ukweli wowote,’’ alisema Hellen.

 

TUJIKUMBUSHE

Miezi kadhaa iliyopita, Diamond kupitia ukurasa wake wa Instagram, aliposti video ikionyesha magari mengi ya kifahari huku akijinadi kuwa ni ya kwake, mbali na hilo, hatukukaa sawa akanukuliwa akisema kuwa, tayari ameshaagiza gari mpya aina ya Rolls Royce toka nchini Uingereza, lakini ilizuiliwa kuingia nchini kutokana na janga la Corona ambalo liliikumba dunia nzima.

Waandishi: Memorise Richard na Happyness Masunga

Leave A Reply