The House of Favourite Newspapers

Magifti Dabodabo Yazidi Kunoga, Wawili Walamba Milioni 5 Kila Mmoja Mwingine Vifaa Vya Hisense

0
Washindi wakiwa mfano wa hundi ya pesa walizojishindia wapili kulia ni Ismail Rashid aliyejishindia vifaa vya Hisense na kushoto ni baba yake mdogo aliyemchagua kama mshindi mwenza ambaye naye anapatiwa seti yake ya vifaa hivyo.

Dar es Salaam, 2 Januari 2024: Kampuni ya mtandao wa simu ya Tigo kupitia kampeni yake ya Magifti Dabodabo leo imeendelea kuwanufaisha watumiaji wa mtandao huo kwa kuwapa zawadi zao washindi wanne waliopatikana wiki hii.

Neema hiyo wiki hii imewadondokea washindi wawili wa milioni tano kila mmoja, mshindi wa shilingi milioni moja na mshindi wa vifaa vya Hisense ambavyo ni seti ya friji, microwave, tv na redio ya muziki mnene (sound bar).

Washindi hao ni Monalisa Lazaro Kasonta, Hemed Swai (Washindi wa milioni tano kila mmoja), Eliva Eliazaro (Mshindi wa milioni moja ) na Ismail Rashid ambaye amejishindia Vifaa vya Ndani kutoka kampuni ya Hisense ambavyo ni tv, friji, redio ya muziki mnene (Sound bar) na jiko la microwave.

Semaji la Magifti Dabodabo Haji Manara (kulia) akimpongeza Baba yake mdogo, Ismail Rashid aliyechaguliwa na mwanaye huyo kama mshindi mwenza wa zawadi ya vifaa vya Hisense (katikati) ni Ismail mwenyewe ambaye ndiye mshindi wa vifaa hivyo.

Kwakuwa vifaa hivyo vinatolewa Dabo dabo kwa mshindi kama lilivyo jina la kampeni hivyo, Ismaili amemchagua Baba yake mdogo, Idd Maulid kama mshindi mwenzake ambaye naye anapewa seti yake ya vifaa kama hivyo.Washindi hao wote walikabidhiwa zawadi zao na Semaji la Kampeni ya Magifti Dabodabo, Haji Manara.

Kampeni hii inaendelea ambapo zawadi kubwa ni Magari mapya ya kisasa ambayo nayo yatatolewa dabodabo kwa washindi ambapo ili ushinde unachotakiwa ni kutumia huduma mbalimbali za Tigo kama vile kununua bado au salio kwa kutumia Tigo Pesa hata vocha za kukwangua, kufanya manunuzi kwa Lipa namba, kulipa bili, malipo mbalimbali ya serikali na nyinginezo.

Leave A Reply