The House of Favourite Newspapers

Magufuli apiga kampeni Singida, Dodoma mpaka Manyara kwa siku moja

0

 

 

magufuli akimpa pole Padre Dk Kitima na familia yake kwa kifo cha mdogo wake kilichotokea hivi karibuni

Magufuli akimpa pole Padre Dk. Kitima na familia yake kwa kifo cha mdogo wake.

mafufuli akiliombea kaburi la marehemu

Magufuli akiliombea kaburi la marehemu.

kijiji cha Siuyu mkoani Singida Magufuli baada ya kutoa kuhani msiba wa mdogo wa Padre Kitima  (1)

…Magufuli baada ya kutoka kuhani msiba wa mdogo wa Padre Kitima.

RPC wa Dodoma David Misime na wa Singida wakikabidhiana majukumu ya kulinda msafara kwenye mpaka wa Singida na Dodoma

RPC wa Dodoma David Misime (kulia) na wa Singida wakikabidhiana majukumu ya kulinda msafara kwenye mpaka wa Singida na Dodoma.

 

kondoa mjini (2)

kondoa mjini (3)

Wakazi wa Kondoa Mjini wakimshangilia Magufuli.

 

Magufuli akiingia babati

Magufuli akiingia Babati.

kondoa mjini (1)

Wakazi wa Babati wakifuatilia kampeni za Magufuli.

Mgombea urais kwa tiketi ya CCM John Pombe Magufuli jana aliuacha Mkoa wa Singinda huku akipiga kampeni katika vijiji kadhaa alivyovibakiza na kurudi mkoani Dodoma katika Wilaya mpya ya Chemba na Wilaya ya kongwe, ambapo alipiga kampeni na kufufua matumaini mapya ya wakazi wa maeneo hayo ambapo alipiga kampeni hizo katika mikutano 15 ikiwemo aliyokuwa akisimamishwa barabarani na wananchi waliokuwa wakiomba ukombozi wake waziri huyo aliyekuwa na sifa ya uchapakazi kwa faida ya wanyonge.

Katika kampeni zake miongoni mwa mambo aliyoyasisitiza Magufuli ni kuondoa kero ya maji ambayo alikutana nayo katika vijiji vingi alivyopita katika mikoa yote mitatu hasa Wilaya ya Chemba na Kondoa.

Baadhi ya vijiji alivyozungumza na wananchi mgombea huyo wa urais ni Siuyu, Makiungu, Misughaa, kinyamshindo mkoani Singida na kuingia Mkoa wa Dodoma katika vijiji vya Likwao,Msera, Kwamtoro, Farkwa, na kuingia Kondoa mjini ambapo alipiga kampeni katika uwanja wa Sabasaba ambapo ulifulika umati mkubwa wa watu.

Baada ya kutoka Kondoa mjini Magufuli alielekea Babati mjini huku akiendelea kusimamishwa na wakazi waliokuwa wakiamini kuwa atawakomboa katika maisha duni na kufika Babati Mkoani Manyara ambapo alipiga kampeni katika uwanja wa Kwaraa ambapo umati mkubwa ulijitokeza kumsikiliza na kuahidi kumpa kura yeye pamoja na wagombea wake wa ubunge na udiwani.

(Habari/ Picha: Richard Bukos)

 

Leave A Reply