The House of Favourite Newspapers

Magufuli Kuhusu Mafuriko: Msiishi Mabondeni, Mtailaumu Serikali – Video

0

RAIS wa Tanzania, John Magufuli amewataka wananchi kujihadhari kujenga nyumba kwenye maeneo ambayo kuna mkondo wa maji.

 

Mkuu huyo wa nchi ametoa tahadhari hiyo leo Jumatano Desemba 18, 2019 wakati anazindua mradi wa Visima vya maji Chato na kuzungumza na wananchi wa Chato katika uwanja wa Shule ya Msingi Chato mkoani Geita.

 

Akitolea mifano ya maeneo ambayo wananchi wamejenga mabondeni, amewataka kuchukua tahadhari wanapojenga nyumba zao ili wasije wakailaumu Serikali badaye.

“Ninajua siku nyingine mvua zinazidi kidogo lakini wakati mwingine tunazichokoza mvua sisi wenyewe mfano pale Sengerema (Mwanza) kuna bwawa linaloteta maji, watu wamelivamia lile bwawa mpaka njia ya kutolea maji kwa kujenga nyumba na maji yamekuja yametuletea madhara mpaka vifo vya watu” amesema.

 

Amesema hata Dar es Salaam kuna watu wamejenga hadi kwenye mto Msimbazi hivyo wasije wakailaumu Serikali.

 

“Hata Dar es Salaam ni hivyohivyo, kwenye maeneo ambayo mito inapita mto Msimbazi nakadhalika watu wamejenga nyumba mpaka mwisho kabisa wa mto.”

 

“Wito wangu kwa Watanzania tujiepushe kujenga nyumba kwenye maeneo ambayo ndio mkondo wa maji au mito, tutaanza kulaumu Serikali, Serikali ndio imekuambia ukajenge kwenye mto,” amehoji Rais.

 

“Sasa jengeni siku mkipelekwa msiseme Serikali, ndio ukweli. Mtu kabla hujajenga kwenye bonde lazima uangalie, bila kufanya hivyo tutakaa tutailaumu Serikali kwa makosa ambayo tunayafanya sisi wenyewe,” amesisitiza.

 

“Na serikali kiukweli itanyamaza, itakuacha tu, haitajibu, kwa sababu saa nyingine mwalimu mzuri ni yule anayekufundisha kwa vitendo” amesema.

Leave A Reply