The House of Favourite Newspapers

Magufuli, Mkewe Wapiga Kura Chamwino -(Picha +Video)

0

ZOEZI la kupiga kura linaendelea katika maeneo mbalimbali nchi nzima, ambapo watu wengi wamejitokeza katika vituo vya kupigia kura tangu asubuhi ya leo Oktoba 28, 2020 ambapo wananchi wanachagua viongozi wanaowahitaji kwa ajili ya kuwatumikia kwa miaka mitano ijayo.

Tayari mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Magufuli amefika katika kituo chake cha kupigia kura Chamwino Ikulu na kupiga kura yake mapema asubuhi hii kumchagua rais na mbunge huku diwani wa kata hiyo akiwa amepita bila kupingwa.

Akizungumza baada ya kupiga kura, Magufuli amesema; “Napenda niwapongeze wasimamizi wa uchaguzi hapa Chamwino; maandalizi yalikuwa mazuri na watu wamejitokeza kwa wingi, wito wangu kwa Watanzania tujitokeze kwa wingi kupiga kura pia nipende kusisitiza amani.”

Leave A Reply