The House of Favourite Newspapers

Mahakama ya Juu Kenya Kufanya Kikao cha Mikakati Kesi ya Kupinga Matokeo ya Urais

0
Majaji wa Mahakama ya Juu zaidi Kenya.

MAHAKAMA  ya juu zaidi nchini kenya imepangiwa kufanya kikao cha kutathmini masuala yatakayoibuka kwenye kesi tisa zilizowasilishwa katika kupinga kutangazwa kwa William Ruto kuwa Rais Mteule.

 

Kwenye tangazo lililotolewa na msajili wa mahakama hiyo, Bi Letizia Wachira, kikao hicho kimepangiwa kuanza leo katika Mahakama ya Milimani.

 

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Idara ya Mahakama, kesi hizo zitaanza kusikilizwa kesho Jumatano na kumalizika Jumapili.

 

Majaji watapumzika kwa siku moja ili kutathmini masuala yatakayowasilishwa na pande zote. Baadaye, watarejea Jumatatu ili kutoa uamuzi wao.

Jaji Mkuu wa Kenya Martha Koome.

Wakati wa kikao cha leo Jumanne, mahakama itaeleza kanuni ambazo zitazingatiwa na walalamishi na mawakili wao.

 

Huku hayo yakiarifiwa majaji watano kutoka mataifa ya kigeni wamefika nchini kufuatilia kesi ya kupinga matokeo ya urais itakayoanza leo saa tano katika Mahakama ya juu

Naibu Jaji mkuu Kenya Philomena Mwilu.

Majaji hao wanachama wa Chama cha Majaji wa Afrika (AJJF), walitua nchini siku ya Jumatatu wakiongozwa na Jaji Mkuu (mstaafu) Mohammed Chande Othman wa Tanzania.

 

Majaji wengine katika ujumbe huo ni Lillian Tibatemwa-Ekirikubinza wa Mahakama ya Upeo Uganda, Ivy Kamanga wa Mahakama ya ya Upeo Malawi, Moses Chinhengo wa Mahakama ya Rufaa Lesotho na Henry Boissie Mbha ambaye ni Rais wa Mahakama ya Masuala ya Uchaguzi Afrika Kusini.

RAIS SAMIA ANAFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA WAKUU WAANDAMIZI NA MAKAMANDA WA POLISI WA MIKOA

Leave A Reply