The House of Favourite Newspapers

Mahakama Yaridhia Kanye West Kubadili Jina

0


Rapa, Mwanamitindo na Mtayarishaji wa Muziki, Kanye West sasa rasmi atatambulika duniani kote kama Ye baada ya Mahakama ya Los Angeles nchini Marekani kuidhinisha ombi lake la kubadili jina.

Kanye Omary West maarufu zaidi kama Kanye West alianza harakati za kutaka kubadilisha jina mapema mwaka 2018 ambapo Agosti, 2021 rapa huyo aliomba kubadili jina lake kuwa Ye baada ya kufungua hati za kisheria na kujaza sababu binafsi za kubadilisha jina.

Hivyo baada ya miaka mitatu, Jaji Michelle Williams wa Mahakama Kuu ya jijini Los Angeles amepitisha ombi la Kanye na sasa Kanye West (Ye)  hatotumia tena majina yake matatu; lake (Kanye),  la baba (Omary) na la ukoo (West).

Rapa huyo mwenye umri wa miaka 44 aliachia albamu yake inayojulikana kama DONDA , Agosti 2021 ikiwa na nyimbo 27 na dakika 108 ambapo ameipa albamu hiyo jina la marehemu mama yake.

Cc; @bakarimahundu

 

Leave A Reply