The House of Favourite Newspapers

Siri za Wabunge Warembo Zavuja, Maisha yao ya Kimapenzi…

0
Mbunge wa Handeni Vijijini (CCM), Mboni Mhita akielezea jambo jimboni kwake.

WAKATI Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivi sasa likionekana kujawa na vijana wengi, wakiwa ni wawakilishi wa majimbo au viti maalum kutoka vyama mbalimbali vya siasa, tofauti na miaka michache iliyopita, siri za maisha ya kimapenzi ya wabunge ‘visu’ imevuja.

Baada ya vijana wa kiume kuanza kuingia bungeni kwa kishindo kuanzia Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2005, katika uchaguzi wa mwisho wa 2015, ongezeko kubwa zaidi limeingia kwa upande wa vijana wa kike, wengi wakiingia kupitia viti maalum na baadhi yao wakipambana majimboni na kuibuka washindi.

Licha ya vijana hao wa kike kuingia bungeni, hata hivyo, baadhi yao wameonekana kuwa warembo zaidi, au kama ilivyo lugha ya mitaani, visu.

Mbunge wa Segerea kupitia Chama Cha M a p i n d u z i (CCM), Bonah Kaluwa.

R i s a s i Mchanganyiko kwa makusudi, liliamua kuw a t a f u t a baadhi ya w a b u n g e hao vijana ambao ni visu na kufanya nao mazungumzo, lakini yakilenga zaidi juu ya maisha yao kimapenzi, hasa kutokana na kazi ngumu ya ubunge, ambayo huchukua muda wao mwingi kiasi ambacho kwa ujana wao huenda kinawaletea shida kwa wenza wao. Baadhi yao, wamekiri kukutana na changamoto mbalimbali katika ndoa na uhusiano wao wa kimapenzi, hii ni kutokana na ubize wa kazi nyingi za kibunge, ikiwemo vikao na majimboni, hivyo wanaume kukosa uvumilivu, jambo ambalo husababisha kuyumbisha uhusiano wa ndoa zao.

MBONI MHITA ANALIANZISHA

Mbunge wa Jimbo la Handeni Vijijini mkoani Tanga, Mboni Mhita alisema miongoni mwa mambo ambayo huwasumbua wabunge wengi vijana hususan wanawake, ni kudumu katika uhusiano wa kimapenzi kutokana na ugumu wa ratiba zao za kazi.

Wabunge wakifuatilia hoja mbalimbali.

Mboni, mwenye umbo na muonekano bomba kwa lugha ya vijana, alisema ni heri ya wabunge wanaume, kwani wanawake huwa wavumilivu na waelewa, lakini shida iko kwa waheshimiwa wanawake kwani wanaume wengi hushindwa kuvumilia hivyo kuteteresha uhusiano wao.

“Nipo kwenye uhusiano, mimi humruhusu patna wangu aje Dodoma wakati wa vikao, ninamkabidhi gari awe kama dereva, anipeleke bungeni na mchana anifuate ili tu ashuhudie namna nilivyo na kazi nyingi.

“Kusema ukweli, shida ipo kubwa sana kwenye uhusiano mwingi kwa wabunge, hususan vijana wa kike, kwani wingi wa kazi huwafanya wapenzi na baadhi ya waume kushindwa kuvumilia ndiyo maana ukifuatilia sana utagundua ndoa nyingi za wabunge zina shida sana, lakini eti wenzetu wa kiume wana unafuu maana wanawake wana uvumilivu.

“Kwa upande wangu, nashukuru sana mwenzi wangu ni muelewa, huwa nalazimika kumuita huku Dodoma, wakati mwingine nampa uhuru wa kuniendesha akinipeleka bungeni na kuja kunichukua, ili aone kabisa namna ambavyo nakuwa na kazi nyingi, lakini sasa wakati mwingine usiri wa baadhi ya wabunge, huwashinda wanaume, mfano sasa unakuwa na mumeo halafu boyfriend naye yupo hapohapo, hiyo sasa lazima ilete shida,” alisema Mboni ambaye kabla ya wadhifa huo, aliwahi kuwa mkuu wa wilaya katika serikali ya awamu ya nne.

HUYU HAPA BONAH MOSES KALUWA

Mbunge wa Segerea kupitia Chama Cha M a p i n d u z i (CCM), Bonah Kaluwa (pichani) ambaye yuko kwenye ndoa, alisema yeye anaishi na familia yake mjini Dodoma ambako Bunge la Bajeti linaendelea na vikao vyake, hivyo hana changamoto za kindoa zinazotokana na shughuli za kibunge. “Mimi niko huku Dodoma na familia yangu, watoto na mume wangu tunaishi pamoja huku, sasa suala la kazi zangu za kibunge kuleta changamoto kwenye ndoa yangu, kwa upande wangu tatizo hilo sina kwa kweli, sijui hao wengine,” alisema.

MSIKILIZE SASA MARIAMU DITOPILE MZUZURI

Mariamu Ditopile Mzuzuri, mtoto wa mwanasiasa wa siku nyingi nchini, marehemu Ditopile Mzuzuri, ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum kupitia CCM akitokea Mkoa wa Dar es Salaam, alikiri kuwepo kwa changamoto, lakini akisisitiza kuwa si kwa wabunge tu, bali watu wote walio kwenye ndoa wanakutana nazo pamoja na matatizo ya hapa na pale. “Unajua mambo hayo bwana (anaangua kicheko) yako pande zote, si kwa wabunge tu, mahusiano yana changamoto nyingi ambazo hazilengi kundi moja la watu, sidhani kama ni sawa sana kutulenga sisi wabunge tu, hayo yako kwa kila pande,” alisema.

NAYE KHADIJA NASSIR ALI

Mbunge Khadija Nassir Ali, kutoka Viti Maalum (CCM) alisema; “Ni kweli, ndoa nyingi za vijana zina matatizo sana, lakini kwa upande wangu mwenzi wangu huwa anakuja huku na kwa mfano kipindi hiki cha likizo ndefu za wanafunzi, kwa hiyo hata familia inakuwa iko huku Dodoma. “Unajua kwa sasa hivi kazi ni nyingi na kila mtu yuko bize, kwa hiyo siyo tu kwamba wabunge ndiyo tuna kazi nyingi zinazoleta changamoto kwenye mahusiano, hata huko mitaani, ndoa nyingi tu za vijana ni matatizo, lakini inategemea na namna ambavyo wahusika wanapanga mambo yao, kwangu mimi muda wa kujiachia
naupata kwa sana tu, kila kitu ni mipangilio, lakini matatizo ya kimapenzi hayakosi.”

AGNES MATHEW MARWA ADAI UVUMILIVU NI TAABU

Agnes, ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum kupitia CCM, akiwakilisha Mkoa wa Mara, alikubali kuwepo kwa matatizo katika ndoa na uhusiano wa wabunge vijana, akisema hali hiyo inachangiwa na kukosekana kwa uvumilivu. Hata hivyo, alisisitiza hali hiyo haiko kwa wabunge tu na kuwataka watu kumshirikisha Mungu
linapokuja suala la kutamfuta mtu wa kutengeneza naye muungano wa kimaisha. “Duh! Ndoa zina matatizo asikuambie mtu, ndiyo maana msisitizo wa kumshirikisha Mungu kwenye suala la ndoa na uhusiano wa uchumba ni mkubwa sana, lakini mbona umeuliza kwa wabunge tu? Kwani walio kwenye ndoa na uhusiano ni wabunge tu? Kila mahali hata huko mitaani hali si shwari, kwa ndoa hususan vijana, mambo yanakuwa mengi,” alisema Agnes ambaye yuko kwenye ndoa.

Leave A Reply