The House of Favourite Newspapers

Majaliwa Afungukia Namungo Kuzuiwa na Jeshi Angola

0

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameipongeza klabu ya Simba kwa kupata ushindi wa kwanza wa bao 1-0 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vital uliochezwa jana jijini Kinshasa DRC Congo.

 

 

Akizungumza bungeni jijini Dodoma leo, Majaliwa amesema hatua hiyo ni mafaniko makubwa kwenye soka hata hivyo ameipongeza Wizara ya Michezo na Shirikisho la soka nchini TFF kwa usimamazi mzuri wa michezo.

 

 

Aidha, Majaliwa amesema kitendo cha timu ya Namungo FC, kuzuiliwa Uwanja wa Ndege ni siasa za soka. Majaliwa amesema Wizara ya Mambo ya Nje inafuatilia kwa ukaribu suala hilo ili kuona namna nzuri ya timu hiyo kucheza mchezo wake wa kombe la Shirikisho kesho.

Leave A Reply