The House of Favourite Newspapers

Majaliwa Awataka Mawakili Na Maafisa Sheria Kuzingatia Weledi

0

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka Maafisa Sheria na Mawakili wa Serikali nchini kutekeleza majukumu kwa kuzingatia weledi, usawa na uadilifu ili kuhakikisha wananchi wanapata haki bila kujali hali zao za kiuchumi.

Majaliwa ameyasema hayo lAlhamisi, Machi 21, 2024 wakati akifugua mkutano wa Mkuu wa Chama cha Mawakili wa serikali Tanzania, uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

Amesema serikali kwa kutambua umuhimu wa upatikanaji wa huduma za kisheria kwa wananchi wote, imeendelea kuchukua hatua kadhaa zikiwemo ujenzi wa miundombinu, uendelezaji wa rasilimali watu, maboresho ya mifumo na sheria mahsusi.

“Hatua hizo zimeendelea kutekelezwa sambamba na kuhakikisha uwepo wa watoa huduma hizo ili ziweze kupatikana pia katika maeneo ya vijijini kwa wananchi walio wengi,”amesema.

katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa amesema Serikali imetekeleza mpango wa ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Mahakama Jijini Dodoma, Vituo sita Jumuishi vya Utoaji Haki, Mahakama za Wilaya 27 pamoja na mahakama za mwanzo 14.

Ameeleza serikali inaendelea na ujenzi wa vituo jumuishi sita vya Geita, Simiyu, Njombe, Katavi, Songea na Songwe.

“Nampongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyoendelea kuimarisha na kuboresha mifumo yetu ya utoaji haki nchini. “Jitihada mbalimbali anazozifanya zinatokana utashi wake katika kuhakikisha misingi ya demokrasia na utawala bora inaimarishwa na kuzingatiwa,”. Ameeleza.

Amesema Rais Dk. Samia ameendelea kuhakikisha huduma za kisheria zinawafuata wananchi pale walipo kwa kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuongeza na kuimarisha miundombinu ya kutolea huduma za sheria.

Majaliwa amesema kutokana na maono na msukumo wa Rais Dk. Samia katika kipindi cha miaka mitatu kwenye tasnia ya sheria na utoaji wa haki,Serikali imewezesha Wananchi 415,280 na mahabusu 7,166 kufikiwa na huduma za kisheria bila gharama kupitia kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia kutoka Mitaa/Vijiji 1,348 kwenye mikoa sita nchini.

Leave A Reply