The House of Favourite Newspapers

Rais Samia, Wizara ya Afya Waipongeza Global TV kwa kuibua habari Ya Mtoto Rama Anayeumwa Figo – “Akatibiwe Bure Muhimbili” – Video

0

Rais Samia Suluhu Hassan kupitia wizara ya afya @wizara_afyatz inayoongozwa na Waziri @ummymwalimu wameipongeza @globaltvonline kwa kuibua habari za kijana Ramadhan Hassan (18) kutoka Tanga ambaye alikwama kupata matibabu kutokana na kukosa fedha.

Kufuatia Global TV kuiripoti habari hiyo, Rais Samia aliguswa na kutoa maelekezo kwa Wizara ya Afya kuhakikisha Ramadhan anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, haraka iwezekanavyo.

“Tunaipongeza Global Tv kwa kuibua habari hii kuhusu kijana huyu mweney uhitaji wa matibabu na sasa Ramadhani Hassan atasafirishwa kuelekea Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi na matibabu bure kwa ugonjwa alionao huku gharama za matibabu yake zitalipwa na Wizara ya Afya,” ilinukuliwa taarifa ya wizara.

Taarifa ambazo Global TV inazo, ni kwamba tayari Ramadhan anapatiwa matibabu hospitalini hapo chini ya uangalizi wa madaktari bingwa wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Leave A Reply