The House of Favourite Newspapers

Majaliwa: Rais Samia Amedhamiria Kulinda Na Kuimarisha Afya Za Watanzania

0

 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia ipo makini na inaendelea kuboresha sekta mbalimbali nchini ikiwemo ya elimu ili kuweka mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia.

Pia, Mheshimiwa Majaliwa amewaagiza Maofisa Elimu wahakikishe wanatenga muda na kwenda katika shule kwa ajili ya kuzungumza na walimu na wanafunzi na kusikiliza kero zao na kushirikiana nao kuzitafutia ufumbuzi badala ya kusubiri ziara za viongozi wa Kitaifa.

Ameyasema hayo  Jumamosi, Novemba 27, 2021  wakati akizungumza na walimu, watumishi wa shule na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kayuki baada ya kukagua na kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa madarasa manne shuleni hapo akiwa katika ziara ya kikazi wilayani Rungwe, Mbeya.

 

“Mheshimiwa Rais Samia ametoa fedha nyingi katika sekta ya elimu ili kuhakikisha shule za msingi na sekondari, vyuo vya elimu ya juu na ya kati vinaboreshwa, hivyo tumieni vizuri miundombinu hii kwa kusoma kwa bidii na mtimize ndoto zenu.”

Kadhalika, Waziri Mkuu ameiagiza Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ihakikishe shule hiyo kongwe inaingizwa katika mpango wa kukarabatiwa kwa kuwa baadhi ya majengo yake ni chakavu. “Pamoja na Serikali kuendelea kuboresha maslahi ya walimu naelekeza shule hii ikarabatiwe.”

Naye, Mkuu wa shule hiyo Mwalimu Bertha Sarufu amemshukuru Mheshimiwa Rais Samia kwa kuwapatia jumla ya shilingi milioni 80 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa. Shule hiyo ya Sekondari ya Wasichana Kayuki ni ya kidato cha kwanza hadi cha sita na ina jumla ya wanafunzi 1,282.

“THAT WAS NONSENSE” – RAIS SAMIA AKASIRIKA, AMLIPUA WAZIRI ALIYEMJIBU VIBAYA RAIS MUSEVENI..

Leave A Reply