The House of Favourite Newspapers

Majambazi Watano Wauawa Wakijaribu Kuteka Gari la Polisi – Video.

0

Watu watano wameuawa na Jeshi la Polisi mkoani Kigoma kwa tuhuma za ujambazi katika Kijiji cha Kitahana Wilayani Kibondo mkoani Kigoma.

 

Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma ACP James Manyama amesema tukio hilo limetokea usiku wa Saa 5 kuamkia leo katika barabara kuu itokayo Kibondo kwenda Kasulu eneo la Kibaoni katika Kijiji cha kitahana.

 

RPC Kigoma akizungumza katika eneo la tukio amesema Majambazi hao walikua wameweka Magogo njiani kwa lengo la kuteka magari barabarani na kwa bahati mbaya gari la kwanza kupita lilikua gari la Polisi ambalo lilikua na namba za Kiraia ambapo majambazi hawakutambua hilo ndipo Askari Polisi walianza mapigano ya kurushiana risasi yaliyosababisha mauji ya watu hao watano ambao huenda kulikuwa na wengine zaidi ambao walikimbia.

 

Katika tukio hilo vitu kadhaa vimekamatwa ikiwemo silaha za kivita ikiwemo mabomu matatu ya kurusha kwa mkono pamoja na silaha za jadi.

 

Ni siku sita tu zimepita baada Jeshi la polisi kigoma kutoa taarifa ya kuwaua Majambazi wengine watatu katika Barabara ya Kagherankanda Mkoani Kigoma.

 

Leave A Reply