The House of Favourite Newspapers

Majembe Mapya Yanga Kutua Kesho

UONGOZI wa Yanga chini mwenyekiti wake DK Mshindo Msolla unaanza kuwapokea nyota wake wapya wa kigeni kesho tayari kwa maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Yanga chini ya kocha Mkongoman, Mwinyi Zahera amefanya mabadiliko katika kikosi chake kwa upande wa nyota wa kimataifa kwa lengo la kuongeza ushindani.

 

Wachezaji hao wataanza kupokelewa kesho na uongozi huo ni pamoja Mnyarwanda, Patrick Sibomana, Sadney Urikhob wa Namibia, Mzambia, Maybin Kalengo, Issa Bigirimana, Mustapha Seleman wote kutoka Burundi.

Yanga inaanza maandalizi ya msimu mpya Julai 7, mwaka huu ikiwa nchini ya kocha msaidizi, Mzambia Noel Mwandila kabla ya Zahera kurejea kutoka mapumzikoni Ufaransa. Chanzo cha kuaminika
kutoka ndani ya Yanga kimeliambia Championi Jumatano kuwa wachezaji hao wanaanza kutua tayari kwa ajili ya kuanza maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa.

 

Championi Jumatano lilitamfuta Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela, alisema: “Ni kweli tunatarajia kuanza kuwapokea wachezaji na mwalimu msaidizi kuanzia kesho.”

Comments are closed.