The House of Favourite Newspapers

Majibu Ya Ukimwi Yamponza Lyyn

0

Majibu yake ya Ukimwi aliyoyaposti mtandaoni, yamemponza video vixen na msanii wa Bongo Fleva, Irene Lous ‘Lyyn’.

 

Baadhi ya mashabiki wake walioyaona majibu hayo, walimjia juu kwa kusema haikuwa na maana kufanya hivyo, kwani ni kutojiamini.

 

Wengine walikwenda mbele zaidi na kusema alifanya hivyo kwa sababu amezoea kutembea na waume za watu  ndiyo maana anakuwa na hofu kila wakati.

 

Hata hivyo, wakati mjadala huo ukiendelea, Gazeti la IJUMAA lilizungumza na Lyyn ambapo kwa upande wake alikiri kuposti majibu hayo na kuongeza kuwa, aliposti kwa faida yake na siyo faida ya mtu mwingine.

Lyyn amewataka watu kuacha kuchonga kwa sababu kila mtu ana uhuru wa kuposti anachojisikia ilimradi tu havunji sheria.

 

“Ni kweli majibu hayo niliposti mimi mwenyewe, kwani ni haki yangu kuposti ninachojisikia.

 

“Mbona hata watu wa kawaida wakienda kupima Ukimwi huwa wanaposti? Mimi niliposti kwa sababu nilijisikia, tena nimeposti kama ambavyo huwa ninaposti picha zangu, sasa sijui watu wanaongeaongea nini,” aliwaka Lyyn ambaye aliwahi kudaiwa kutoka kimapenzi na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.

Leave A Reply