The House of Favourite Newspapers

Majizzo Aanika Mazito: Walisema Pete Itakata Kidole

0

 

HATIMAYE Mkurugenzi Mtendaji wa Efm Radio na ETV, Francis Antony Ciza a.k.a Majizzo amefunguka kwa mara ya kwanza ikiwa ni siku 15 baada ya kufunga ndoa na msanii maarufu wa Bongo Movies,  Elizabeth Michael ‘Lulu’.

 

 

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Majizzo ameandika waraka huu:

 

 

Imenichukua muda kuyasema haya, baada ya shughuli nyingi za kitaifa naomba niyaseme leo. Kwanza ni shukrani kwa kila mtu aliyehusika kufanikisha ndoa yangu na mke wangu Eliza.

 

 

Ndugu, marafiki na jamaa wote asanteni sana. Nawashukuru kwa namna mlivyonielewa hasa katika style tuliyochagua kufunga ndoa yetu, imenipa faraja kuona watu wangu wote wamekuwa waelewa na kulipokea positively. Asanteni.

 

Lakini kipekee sana shukrani zangu ni kwa Mke wangu. Namshukuru kwa namna alivyokuwa muelewa nyakati zote, alikuwa mhanga wa maneno, matusi, kejeli na yote aliyopitia kutokana na mahusiano yetu.

 

 

Aliambiwa ana uchumba sugu, mara pete inakata kidole 😄, lakini yote hayo hayajawahi kumtia unyonge wala kumtoa kwenye mstari wa kile tunachoamini sisi. Hajawahi kunipa presha, hajawahi kuonesha dalili za kukosa subra kwa kuwa mimi na yeye tulijua ni nini tunafanya.

 

 

Naomba spirit hiyo iwe funzo kwa wadogo zangu wanaowaza kuoa au kuolewa, tembeeni kwenye njia yenu, fanyeni mambo kwa wakati mnaotaka ninyi huku MKIMTANGULIZA MUNGU. Msiyumbishwe na maneno ya watu, na Mungu atawasaidia.

 

Again, asanteni kwa pongezi, asanteni kwa ushauri na kila kitu. Mungu azidi kutubariki sote. Oya Mama G, @elizabethmichaelofficial, umetisha sana. 👊🏼

Leave A Reply