The House of Favourite Newspapers

MAJUTO: SITAKI KUFA NA MTU

0
MAJUTO: SITAKI KUFA NA MTU
Mzee Majuto.

KOMEDIANI mwenye jina kubwa Bongo, Amri Athuman ‘Mzee Majuto’, amevunja ukimya kuwa, katika umri alionao kwa sasa wa zaidi ya miaka sitini, hataki kulumbana na mtu maana siku zake za kuishi zimebaki chache asije akafa na mtu.

Akizungumza na Ijumaa  Wikienda, Mzee Majuto alisema kuwa, kitu ambacho anakiepuka kwa sasa ni kugombana na mtu na ndiyo maana hata akisemwa vibaya kwenye mitandao ananyamaza kwani umri umemtupa mkono.

“Siku zangu za kuishi zimebaki chache na huu uzee, ninatafuta nini kuanza kugombana na vijana wadogo? Hata watu wazima wezangu? Siku zangu za kuishi zimebaki chache, nisije nikafa na mtu bure,” alisema Mzee Majuto.

STORI: IMELDA MTEMA| IJUMAA WIKIENDA

=====

VARANGATI: Mgomo wa Daladala DAR Yasimama, Madereva Watoa Yamoyoni

Usipitwe na Matukio, Install ===>Global Publishers App

Leave A Reply