The House of Favourite Newspapers

Makambo Amtaka Ibrahim Ajibu

0

STRAIKA wa Horoya AC ya Guinea, Mkongomani, Heritier Makambo, amefunguka kuwa beki Kelvin Yondani na straika Ibrahim Ajibu ni watu anaotamani kucheza nao pamoja.

 

Staa huyo ambaye alipita Yanga na kufunga mabao 17 katika Ligi Kuu Bara 2018/19, ameweka wazi kwamba licha ya kuwa na orodha ndefu ya wachezaji ambao anatamani kucheza nao lakini anajisikia vizuri akicheza na wawili hao.

 

Kabla ya kusajiliwa na Horoya AC, Makambo alicheza na Yondani na Ajibu na kuifanya Yanga kumaliza nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu Bara msimu uliopita.

Makambo amesema kuwa anajisikia vizuri akiwa anacheza na wachezaji hao wawili ambapo anatamani acheze nao tena licha ya kwamba wapo wengi ambao alicheza nao kwenye kikosi hicho.“Kama nikiambiwa nichague wachezaji ambao natamani kucheza nao basi ni Ajibu na Yondani kwani kama nacheza na wachezaji hao najisikia vizuri.

 

“Wapo wengi ambao nimecheza nao kama Feisal Salum ‘Fei Toto’ lakini hao wawili ndiyo ambao naweza kuwachagua kucheza nao kwa mara nyingine ile,” alimaliza straika huyo anayehusishwa kurejea Yanga kwa msimu ujao.Kwa msimu huu akiwa na Horoya, Makambo amecheza katika mechi 10 za ligi ya nchi hiyo na akifunga mabao mawili pekee.

Stori: Said ally, Championi Jumamosi

Leave A Reply