The House of Favourite Newspapers

Maelfu Wafurika Kampeni za Mama Samia Kigamboni

0
Mgombea Mwenza wa Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan (kushoto) akihutubia maelfu ya wakazi wa Kigamboni jijini Dar es Salaam. Kulia ni mgombea ubunge jimbo la Kigamboni,Dkt. Faustine Ndungulile akionesha ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mgombea Mwenza wa Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan ameendelea na ziara ya kuomba kura kupitia Chama Cha Mapinduzi mapema leo katika viwanja vya Mji Mwema, Kigamboni jijini Dar.

Akizungumza wakati wa mkutano huo Mh.Suluhu amesema  kuwa  miradi yote ambayo Chama Cha Mapinduzi iliyoahidi imetekelezwa na bado inaendelea nayo.
 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwahutubia wananchi wa Kigamboni.

“Tumetekeleza miradi mingi ya Kigamboni na ninawaomba tarehe 28 Tukamilishe kazi iliyokusudiwa kwa kuwa miradi mingi imetekelezwa katika Serikali ya awamu ya tano na nyie ni mashuhuda wa maendeleo yaliyofanyika na ilani imetekelezwa kwa kufanya yote tuliyoyahidi sehemu nyingine yamekamilika na sehemu nyingine yanaendelea.

 

Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM na Wananchi wa Wilaya ya Kigamboni  Jijini Dar es salaam wakimsikiliza Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, alipokuwa akiwahutubia kwenye mkutano wa kampeni wa Chama Cha Mapinduzi katika Uiwanja vya Zamani wa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mji Mwwema Dar es Salaa.

“Tumeweza kutumia mamilioni ya fedha kwa ajili ya watoto wa shule za msingi na Sekondari kwenye elimu bure na ujenzi wa matundu ya vyoo kwa ajili ya watoto,tumeongeza fedha kwa watoto wetu wa elimu ya juu na miundo mbinu itaendelea kukarabatiwa. Tunakwenda kuimarisha elimu ya watu wazima ili waweze kujua kusoma na kuandika.

 

…Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wasanii wa kikundi cha Mama Ongea na Mwanao alipowasili Uwanja wa Ofisi ya Zamani ya Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni  Mji Mwema.

 

“Tumejenga Barabara na madaraja na tutendelea kuimarisha na kujenga barabara za juu 8 ikiwemo  barabara za magari yaendayo kasi, kwenye usafiri wa Reli na Ndege pia ujenzi wa Barabara za juu katika maeneo ya Uhasibu, Moroco, Mwenge, Kamata.

“Changamoto ya maji tutaimaliza kwa kuwa tumeshaikabidhi Dawasa baada ya miaka miwili hakutakuwa na changamoto hiyo tena.

Ninawaombee kura Madiwani,pamoja na Mbunge kura ziwe nyingi ili tuweze kusukuma gurudumu la maendeleo,” amesema.

 

Aliyekuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chadema Kadawi Lucas Limbu akirudisha kadi iliyokuwa yake ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambae pia ni Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, baada ya kuamua kukihama Chama hicho na kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM  leo Septemba 08, 2020.

Naye mgombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi Dkt. Faustine Ndungulile amesema kuwa miradi yote imetekelezwa kwa mujibu wa Ilani ya Chama.

“Tunatarajia kutakuwa na soko kubwa katika wilaya yetu ambayo itasaidia wananchi waweze kupata bidhaa hapo na kujipatia kipato.

“Kauli mbiu ni Ndungulile mitano tena kwa kuwa mimi nimesimamia nitawalipa maendeleo mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ndio maana miradi yote ambayo tuliihaidi tumeitekeleza ikiwemo ujenzi wa Hospitali,vituo vya Afya,” amesema.

Leave A Reply