Makamu wa Rais Mpango: Mitambo Miwili ya Kuzalisha umeme katika Bwawa la JNHPP Itawashwa
Makamu wa Rais Dk Philip Mpango, amesema mwezi Machi mwaka huu itawashwa mitambo miwili ya kuzalisha umeme katika Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere (JNHPP), ambayo itasaidia kumaliza makali ya changamoto ya ukosefu wa umeme nchini.
Amesema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Kabuku wilayani Handeni, akiwa njiani mkoani Taga ikiwa ni ni siku ya kwanza ya ziara yake mkoani humo.
Amesema walikuwa wamejipanga kuwasha mtambo mmoja mwezi huu, lakini wameona ni vyema wasubiri mpaka mwezi ujao, ndio waweze kuwasha mitambo miwili ambayo itaimarisha hali ya upatikanaji wa huduma hiyo.
“Ule mradi wetu wa kuzalisha umeme, umefikia hatua nzuri, ilikuwa tufungue mtambo mmoja lakini sasa tunakwenda kufungua mitambo miwili toka kwenye bwawa letu jipya,”amesema Dk Mpango.