The House of Favourite Newspapers

Makamu Wa Rais Samia Ahutubia Maadhimisho Ya Siku Ya Magonjwa Adimu Dunia -Video

0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia Taifa kwenye Maadhimisho ya siku ya Magonjwa Adimu Duniani yaliyoadhimishwa leo Februari 28,2021 katika Ukumbi wa Serena Jijini Dar es salaam. Ambapo kauli mbiu ya Maadhimisho ya Mwaka huu Siku ya Magonjwa Adimu ni “Usawa kwa Waishio na Magonjwa Adimu”.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimtunuku Tuzo Mhe. Faustine Ndungulile Waziri wa Sayansi na Teknolojia ya Habari kwa kutambua mchango wake uliotukuka katika kusaidia Ustawi wa Watoto wenye Magonjwa Adimu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimtunuku Tuzo Ndugu. Ally Khamis Juma Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kwa Niaba ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kwa kutambua mchango wake uliotukuka katika kusaidia Ustawi wa Watoto wenye Magonjwa Adimu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitunuku Tuzo kwa Muwakilishi wa Kituo cha Clouds TV Babbie Kabae kwa kutambua mchango Uliotukuka kwa Kituo hicho kuweza kutoa Habari katika kusaidia Ustawi wa Watoto wenye Magonjwa Adimu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimtunuku Tuzo Getrude Elias Maruma Mwanafunzi wa Chuo cha IFM kwa kuweza kujitokeza Hadharani kuelezea juu ya tatizo la Ugonjwa Adimu

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amehutubia Taifa kwenye Maadhimisho ya siku ya Magonjwa Adimu Duniani yaliyoadhimishwa leo Febuari 28, 2021 katika Ukumbi wa Serena Jijini Dar es salaam. Ambapo kauli mbiu ya Maadhimisho ya Mwaka huu Siku ya Magonjwa Adimu ni “Usawa kwa Waishio na Magonjwa Adimu”.

Leave A Reply