The House of Favourite Newspapers

Makonda Aahidi Kuendeleza Miradi ya Vijana Dar

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akiongea na wanahabari katika mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Kivule.

MKUU wa Mkoa wa Dar es  Salaam, Paul Makonda, ameendelea na ziara ya kukagua miradi ya serikali inayojengwa kupitia fedha za Manispaa, za kimkakati na maendeleo ya wadau ili kukamilisha ilani ya Chama Cha Mapinduzi ambayo inatakiwa kuwa imekamilika kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ambapo pia ameahidi kuendeleza miradi ya vijana wajasiriamali.

 

Makonda alikuwa katika ziara iliyomfikisha katika mradi wa ujenzi wa Soko la Kisutu, mradi wa ujenzi wa Barabara ya Swahili eneo la Gerezani, Kariakoo,  ujenzi wa barabara eneo la Gongo la Mboto nyuma ya  Chuo cha Kampala na ujenzi wa Hospitali ya Kivule.

…Akiendelea na ukaguzi wa mradi huo.

Akizungumza na Global Publishers, Makonda amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Sophia Mjema, kwa kazi nzuri iliyofanyika katika ujenzi wa Hospitali ya Kivule Wilaya ya Ilala.

 

“Nampongeza Mkuu wa Wilaya kwa kusimamia ujenzi wa Hospitali ya Kivule unaoendelea vizuri na mwisho wa mwezi wa sita itakuwa imekamilika kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa hali ya chini, na itakuwa Hospitali ya Wilaya ya Ilala,” alisema Makonda.

Taswura nyingine ya mradi huo unaoendelea.

Alisisitiza kwamba Rais John Magufuli anataka kuona huduma zinamfuata mwananchi na siyo mwananchi anaifuata huduma na akaongeza kwamba hospitali hiyo itatumika kwa wananchi wote ambao walikuwa wakienda katika Hospitali  ya Amana ambao wanaoshi maeneo hayo.

Jengo mojawapo la mradi huo.

Aidha Mkuu wa Mkoa huyo  ametoa ahadi kwa vijana wanaochomelea na kuuza vyuma wa maeneo ya Gerezani/Swahili kuwaendeleza katika Chuo cha Ufundi Veta ili kuukuza ujuzi wao na kupata vyeti vinavyotambulika na serikali.

Stori:Neema Adrian, Global Publishers

 

Comments are closed.