The House of Favourite Newspapers

MAKONDA: DAR NDILO JIJI LA RAHA TANZANIA – VIDEO

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemhakikishia Rais John Magufuli kuwa mkoa huo upo shwari wala hakuna ‘vurugu’ za kupandisha holela bei ya vyakula kama ambavyo imekuwa ikifanyika miaka ya nyuma kwenye kipindi kama hiki cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

 

Makonda ameyasema hayo leo Alhamisi Mei 17, 2018 wakati akitoa salam kwa Rais Magufuli wakati wa uzinduzi wa kituo cha uwekezaji cha Jeshi la Wananchi Tanzania, JWTZ uliofanyika katika eneo la Mgulani jijini Dar.

“Mhe. Rais, nakuhakikishia Jiji la Dar lipo shwari, amani ipo, chakula kipo cha kutosha, kuanzia sukari, mafuta, tambi hadi mihogo na vyote vinavyohitajika kwa ajili ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhani, maduka yataongezewa muda wa kufungwa hadi saa sita usiku ili wananchi wajipatie mahitaji yao. Dar ndilo jiji la raha hapa Tanzania,” alisema Makonda.

Aidha, Makonda alimshukuru Rais kwa kuusaidia Mkoa wa Dar kupatiwa mabilioni ya fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo kipya na cha kisasa cha mabasi yaendayo mikoani kinachotarajiwa kujengwa Mbezi Louis, vituo vingine vya mabasi na daladala, soko la kisasa la Kisutu, ujenzi wa uwanja wa ndege Terminal 3, barabara za juu (fly overs) na machinjio ya kisasa eneo la Vingunguti.

 

Katika hafla hiyo, RaisĀ  amezindua kituo cha uwekezaji cha JWTZ kupitia SUMA-JKT kilichopo Mgulani Jijini Dar es Salaam. Kituo hiki kina kiwanda cha Ushonaji, Maji, Chuo cha Ufundi Stadi, Shule ya Sekondari Jitegemee na Ukumbi wa Mikutano.

 

Comments are closed.