Mama Samia: Serikali Kuendeleza Miradi ya Maji ‘Kumtua Mama Ndoo Kichwani’ – Video
LEO Machi 8, 2020 ni siku ya Kimataifa ya Wanawake siku ambayo dunia inathamini mchango wa Wanawake katika jamii huadhimishwa tarehe 8, Machi ya kila mwaka na kauli mbiu ya mwaka huu ni “Kizazi cha Usawa kwa Maendeleo ya Tanzania ya Sasa na Baadae”.
Maadhimisho hayo kitaifa yamefanyika Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Simiyu mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ameitaka Halmashauri ya Mji wa Bariadi kutumia mapato yatakayotokana na stendi mpya ambayo inatarajia kukusanya mililoni 300 kwa mwaka katika shughuli za maendeleo ya wananchi.
Katika hotuba yake Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ameyasema haya;-
“Tuliwapa maelekezo Benki ya Posta kufungua dirisha maalum kwa ajili kuwahudumia wanawake kama ilivyokuwa benki ya wanawake na wanafanya vizuri, kati ya Agosti 2018-Machi 2019 zaidi ya Tsh Bil. 2 zimetolewa kwa wanawake wajasiriamali.