Mama Wa Mapacha Aliyekuwa Amezuiwa Hosptalini Arusha Alipiwa Bili – Video
Mwanadada Mwanaidi Seleman ambaye alijifungua watoto mapacha ambao hawajatimia muda wao (njiti) katika Hospitali ya Selian Lutheran iliyopo Arusha kisha kuzuiliwa na uongozi wa hospitali hiyo kwa sababu ya kudaiwa kiasi cha shilingi milioni 1.6, hatimaye ameruhusiwa kutoka na wanaye baada ya msamaria mwema kumlipia deni hilo.