The House of Favourite Newspapers

Msaidizi wa Membe Anashikiliwa na Polisi – Mambosasa

0

KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa, leo Septemba 17, 2020, amesema msaidizi wa mgomba urais kupitia chama cha ACT Wazalendo, Bernard Membe, aitwaye Jerome Luanda, yuko mikononi mwa polisi akiwa ni mzima wa afya na hakutekwa.

 

Amesema hayo akiwa anazungumza na East African Radio ya jijini Dar es Saalam, ambapo amethibitisha  msaidizi huyo  alikamatwa  Uwanja wa  Ndege wa Kimataifa wa  Julius Nyerere, Dar es Salaam na akakanusha habari za kutekwa.

 

“Huo ni uongo na uzushi; tumemkamata akiwa airport pale Julius Nyerere, nasikia wengine wanasema wamemtafuta vituo vyote hawajamuona.  Ni uongo, sisi tupo naye na ni mzima wa afya, tunamshikilia kutokana na kesi zake ambazo hatuwezi kuzitaja,” amesema na kuongeza:

 

“Na huyu nasema amekamatwa, anatuhumiwa kwa kosa la kutakatisha fedha, kwa hiyo anayetaka kuthibitisha hilo ni suala la kuja tumueleze ukweli wa jambo hilo.”

 

Tukio hilo limejiri baada ya mgombea urais huyo, kuandika katika ukurasa wake wa Twitter Septemba 16, 2020,  kuwa msaidizi wake amechukuliwa na watu wasiojulikana, na hivyo akatoa masaa kadhaa ili awe amepatikana.

Leave A Reply