The House of Favourite Newspapers

Mamia Wamzika Akilimali wa Yanga Tandale Dar (Picha +Video)

0
Maziko yakiendelea katika Msikiti wake wa Baraqat uliopo Tandale jijini Dar es Salaam.

MAZIKO  ya aliyekuwa Katibu wa Baraza la Wazee la Yanga, Ibrahim Akilimali  yamefanyika leo Desemba 15, katika Msikiti wake wa Baraqat uliopo Tandale jijini Dar es Salaam baada ya kufikwa na umauti Jana Jumamosi, Desemba 14, 2019 katika Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo.

Umati wa wananchi wakiwa wamebeba mwili wa Katibu wa Baraza la Wazee la Yanga, Ibrahim Akilimali. 

Katika maziko hayo ya Mzee Akilimali yalihudhuriwa na mamia ya watu wakiwemo mashabiki, wachezaji, viongozi wa klabu za Simba na Yanga pamoja na viongozi wa kisiasa.

 

Yanga alikuwepo Mwenyekiti wa klabu hiyo, Dk Mshindo Msolla, Katibu Mkuu, Dk David Ruhago na Ofisa Mhamasishaji, Antonio Nugaz.

Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla (wa pili kutoka kulia) akiwa na Katibu Mkuu, Dk David Ruhago (kulia).

Wengine ni aliyekuwa Mratibu wa timu hiyo, Hafidh Saleh pamoja na wanachama mbalimbali. Kwa upande wa Simba alikuwepo mwenyekiti wa zamani wa timu hiyo, Hassan Dalali na aliyekuwa Mbunge wa zamani wa Kinondoni, Idd Azzan.

Jeneza lililobeba mwili wa Ibrahim Akilimali likitolewa kwa ajili ya kuelekea kuzikwa.
Mashehe wakisoma dua kabla ya mwili kwenda kuzikwa
Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali akiwa msibani hapo
Leave A Reply