The House of Favourite Newspapers

Man United Yakwama Kwa Eriksen

MANCHESTER United imekwama katika harakati za kutaka kumsajili staa wa Tottenham Hotspur, Christian Eriksen. Dili hilo limekwama kutokana na kitendo cha Tottenham kutaka dau zito la pauni milioni 80 (Sh. bilioni 223) ili kumwachia staa huyo wa timu ya taifa ya Denmark.

 

Tottenham inasemekana mara ya kwanza walikuwa tayari kupokea pauni milioni 60 (Sh. bilioni 167.3) lakini ilipotokea Manchester United wakapandisha dau. Eriksen inasemekana anataka bado anataka kuondoka Tottenham licha ya ukweli kuwa dirisha la usajili England linafungwa. Hata hivyo, mkazo wa staa huyo ni kutaka kuhamia Real Madrid ambapo bahati nzuri dirisha la usajili kwa nje ya England linafungwa Septemba 2, mwaka huu.

 

Medani ya soka majuzi ilitawaliwa na taarifa juzi za Manchester United kumfukuzia Eriksen. Eriksen bado anataka kwenda Real Madrid ingawa pia anaangalia uwezekano wa kujiunga na Atletico Madrid au Juventus

Comments are closed.