The House of Favourite Newspapers

Manara awatolea povu TFF

AFISA HABARI mwenye mbwembwe nyingi kuliko wasemaji wengine wa timu za hapa nchini, Haji Manara wa Simba, ameibuka na kuweka bayana kwamba Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limejipa mzigo mzito wa kuubeba msimu ujao kutokana na wingi wa timu ambazo zitashiriki ligi kwa msimu wa 2018/19.

TFF waliongeza timu am­bazo zitashiriki ligi kuu kwa msimu ujao kutoka 16 za sasa hadi 20 ambapo timu sita zilipanda kutoka Ligi Daraja la Kwanza msimu uliopita. Timu hizo ni JKT Tanzania, African Lyon na KMC za Dar, Biashara United ya Mara, Coastal Union ya Tanga na Alliance ya Mwanza.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Manara amesema kwamba anaona TFF watakuwa na kazi kubwa kutoka­na na changamoto ya viwanja ambavyo vingi siyo rafiki kwa kuchezea sam­bamba na tatizo la ratiba ambayo ime­kuwa ikib­adilishwa kila mara.

“Kwangu naona kwamba kwa msimu ujao TFF watakuwa na kazi kubwa ya kufanya hasa baada ya kuongeza timu ambazo zitakuwa kwenye ligi kuu.

“Kuwa na timu 20 katika ligi siyo jam­bo dogo tena katika sehemu ambayo ina changamoto kubwa ya viwanja ambapo vingi vimekuwa siyo rafiki kwa wachezaji kucheza.

“Lakini kwa sasa tu tumekuwa tukiona juu ya hali ya upanguliwaji wa ratiba kwa kila mara tena zikiwa timu 16 sasa zinapokuja timu 20 si kutakuwa na matatizo zaidi, kwangu naona kama TFF watakuwa na kitu cha ziada ambacho wa­natakiwa wakifanye katika maeneo hayo ili ligi iwe nzuri,” alisema Manara.

Said Ally, Dar es Salaam.

Comments are closed.