The House of Favourite Newspapers

Mapokezi Ya Makonda Yatikisa Dar, Akabidhiwa Ofisi Kwa Mara Ya Kwanza (Picha +Video)

0
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda, akipokelewa rasmi katika ofisi ndogo za chama hicho, Lumumba jijini Dar es Salaam baada ya kuteuliwa siku kadhaa.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda, leo Oktoba 26, 2023 amepokelewa rasmi katika ofisi ndogo za chama hicho, Lumumba jijini Dar es Salaam baada ya kuteuliwa siku kadhaa zilizopita ambapo amefika akiwa anaendesha bodaboda na kusindikizwa na mamia ya wafuasi wa chama hicho.

Amesema hana kinyongo na mtu na kamwe hatalipa kisasi kwa mtu yeyote kwani hiyo siyo kazi aliyoteuliwa kuifanya.

“Dokta Samia Suluhu Hassan ana R zake nne, na tangu niteuliwe nimepata nafasi ya kupitapita kwenye mitandao nimesoma maoni ya baadhi ya watu, wengi wanahamaki na wengi wanabashasha, na waonaohamaki wengi wao wanawaza tu Makonda ataenda kulipa kisasi…”

Leave A Reply