The House of Favourite Newspapers

Mangula: Tusikate Tamaa, Mambo Yatakuwa Kama Ilivyopangwa – Video

0

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Philip Mangula ameeleza mafanikio wakati wa utawala wa Dk John Magufuli yalitokana pia na utamaduni ambao aliujenga wa kukutana na wajumbe wa Kamati Kuu kutafakari maendeleo ya nchi.

 

 

Mangula alisema akiwa Mwenyekiti wa CCM, Dk Magufuli alikuwa anakutana na wajumbe hao wa chama kila baada ya miezi minne.

 

 

Pia alikutana na wajumbe wa Halmashauri Kuu kila baada ya miezi sita na kujadili kuhusu maendeleo na hatua za kuchukua kuondoa changamoto zinazozuia maendeleo ya haraka ya nchi.

 

 

Mangula alisema kutokana na utamaduni huo, wajumbe wenzake waliobaki watamkumbuka kwa juhudi zake na umahiri wa kuunganisha chama na kuwa wamoja katika kukabili changamoto na kuleta maendeleo endelevu katika nchi.

 

 

Alisema chama pia kilijenga utaratibu wa kuandika taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi mara mbili kila mwaka kuangalia utekelezaji ulivyofanikiwa ili kurekebisha mahali penye matatizo na kuboresha mahali palipoenda vizuri.

 

 

“Anayeandika taarifa ya utekelezaji ni Waziri Mkuu kwa niaba ya serikali, kwa nini nayasema haya, ni ili tusikate tamaa na kujiuliza sasa itakuwaje baada ya kiongozi wetu kututoka,” alisema Mangula.

 

 

Mangula aliwataka Watanzania wote kutokata tamaa kwa kuwa mambo yote yaliyoanza kutekelezwa na Magufuli yanatoka katika ilani hivyo Rais aliyechukua nafasi, atayapeleka kwa umakini uleule.

 

Tusikate tamaa…. ilani ni ile ile, tofauti ni kasi na ubunifu wa kutenda, hakufanya peke yake, alifanya na wasaidizi wake, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Baraza la Mawaziri… tuseseme kwamba sasa itakuwaje, hapana, itakuwa kama ilivyopangwa, amekwenda kamanda wetu, tumesononeka sana.

 

“Bahati nzuri Makamu wa Rais wakati huo ambaye sasa ni Rais wetu ni mjumbe wa Kamati Kuu ulishiriki kikamilifu kuzunguka na kunadi kwa wananchi ilani hiyo yenye kurasa 303 na najua wakati wote umekuwa ukiangalia na kuona mwenendo wa kikao chako kile,” alisema.

 

 

Alisema kwa kuwa Samia anashika usukani na wajumbe wake ni walewale wa enzi za Magufuli, tofauti ni kasi na ubunifu katika utendaji hivyo hakuna kitu kitakachopwaya.

 

 

Aliwaomba viongozi wa CCM pamoja na viongozi wengine wanaohusika katika kuendesha miradi na maendeleo ya nchi kutoingia hofu na kuogopa kwamba sasa itakuwaje.

 

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers)

Leave A Reply