The House of Favourite Newspapers

Meli ya Evergreen Yakwama na Shehena ya Mizigo

0

Meli ya ‘Ever Green’ inayomilikiwa na Kampuni ya ‘Evergreen Marine Corporation’ kutoka nchini Taiwan imekwama katika mfereji wa ‘Suez’ uliopo nchini Misri ambao unatenganisha Afrika Mashariki ya Kati na Asia hali inayozuia meli zingine zenye bidhaa za mafuta na makontena kushindwa kupita na kusababisha hasara ya Dola bilioni 10 kwa siku.

 

Meli hiyo ilikwama siku nne zilizopita ambapo taarifa zinaeleza kuwa licha ya juhudi za kuivuta zoezi limekuwa gumu na huenda likafanikiwa baada ya wiki kadhaa kwa lengo la kuirudisha kwenye mkondo huku zaidi ya meli 200 zikishindwa kusafirisha bidhaa za mafuta na nyinginezo kwa tangu Jumanne.

 

Meli hiyo inauzani wa tani 200,000 na uwezo wa kubeba makonteni 20,000 kwa safari moja, bidhaa zilizokwama kufuatia tukio hilo ni mafuta na bidhaa za nyumbani kama vile, samani, na vipuri vya magari.

 

 

Ripoti za takwimu zinaeleza hali hiyo inasababisha hasara nyingine ya Dola milioni 400 kwa saa ambazo zingepatikana kutokana usafirishaji wa bidhaa zingine.

Leave A Reply