Kartra

Manula Kuikosa Al Merrikh? Kocha Afunguka

 

KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema kuwa anaamini kipa wake namba moja Aishi Manula atakuwa sehemu ya kikosi kitakachowafuata Wasudan, Al Merrikh ambao watacheza nao Machi 6, kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Manula aliumia jana Machi Mosi kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya JKT Tanzania, dakika ya 67 wakati akiokoa mpira uliokuwa ukielekea langoni mwake baada ya kugongana na mshambuliaji Lyanga Daniel.

 

 

Gomes ambaye alikiongoza kikosi chake kushinda mabao 3-0 na kusepa na pointi tatu muhimu ameweka wazi kwamba kipa huyo ni muhimu ndani ya kikosi chake.

 

 

Dakika ambazo zilibaki langoni alikaa kipa namba mbili Beno Kakolanya ambaye aliendelea pale ambapo Manula ameishia kwa kuokoa hatari zilizokuwa zikienda langoni mwake.

 

 

“Baada ya mchezo kuisha daktari ameniambia kuwa kila kitu kipo sawa, amepelekwa hospitali ili kufanyiwa vipimo na tunasubiri majibu. Manula,(Aishi) ni mchezaji muhimu sana na nina uhakika ataweza kucheza Sudan,”.

 

 

Ipo kundi A ndani ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo imetinga hatua ya makundi na inaongoza kundi hilo ikiwa na pointi sita.

 

 

Ina mtihani wa kusaka pointi tatu ugenini mbele ya Al Merrikh ambayo ina hasira kwa kupoteza mechi zake zote mbili ilizocheza.

 

 

Leo Machi 2 kikosi cha Simba kinatarajiwa kuanza safari kuelekea nchini Sudan kwa ajili ya mchezo huo muhimu ambao utakuwa na ushindani mkubwa ndani ya dakika 90.

 

 

Kwenye mechi zote za kimataifa kuanzia ile ya hatua ya awali dhidi ya FC Plateau ya Nigeria wakati Simba ikishinda kwa bao 1-0 ugenini na kwa Mkapa ngoma kuwa 0-0 Manula alikaa langoni.


Toa comment