Kartra

Kipa Yanga Amkingia Kifua Sarpong

KIPA namba mbili wa kikosi cha Yanga, Faroukh Shikhalo amesema kuwa anaamini mshambulijai wao Michael Sarpong ana uwezo mkubwa ambao unahitaji muda kuonekana ndani ya uwanja.

 

Sarpong ambaye ni ingizo jipya ndani ya Yanga yeye ni raia wa Ghana aliibuka kwenye kikosi hicho kinachonolewa na Cedrick Kaze kwa dili la miaka miwili akitokea Klabu ya Rayon Sports ya Rwanda.

 

Ndani ya Yanga ambayo inaongoza ligi ikiwa na pointi 49 kibindoni baada ya kucheza mechi 21 na imetupia jumla ya mabao 34. Amehusika kwenye mabao sita, amefunga mabao manne, pasi moja ya bao na amesababisha penalti moja.

 

Idadi hiyo ni sawa na yale mabao ambayo amefunga nahodha wa timu hiyo Lamine Moro huku msaidizi wake Bakari Mwamnyeto akiwa ametupia bao moja.

 

Shikhalo amesema:” Akiwa kwenye mazoezi anafanya vizuri na anapata nafasi ya kufunga hivyo kinachomkuta ndani ya uwanja ni presha ya kufunga, jambo ambao linamfanya ashindwe kuonyesha uwezo wake.

 

“Ni suala la muda kwamba atakuwa sawa na siku ambayo atafunga itakuwa furaha kwake na timu kiujumla,”.

 

Machi 4 kikosi cha Yanga kina kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.


Toa comment