The House of Favourite Newspapers

Mapazia Ya Chumbani -9

0

ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA:

Mzee Mashali akiwa katika kuwaza na kuwazua bila kujua atatoka na viatu gani mule ndani, ghafla jicho lake likatazamana na sendozi za kijani zikiwa zimenyanyuliwa juu na mama Muro. Hakutaka kuamini macho yake.

“Ina maana mama Kirumba alienda na sendozi zangu?”

ENDELEA NAYO MWENYEWE…

Bado mzee Mashali hakutaka kabisa kukubaliana na ukweli wa kile alichokuwa amekishika mama Muro mkononi. Akatoka katika eneo la dirishani na kutafuta sendozi zake kwa mara nyingine.

Akavuta fuko lake la rambo lililokuwa limejaa mapazia pembeni ya mlango. Kitendo cha kuliinua lile fuko akaziona sendozi zake za kijani.

‘Ohhh!, Kumbe mtu unaweza kufa kwa presha hivihivi unajiona,” alijisemea mzee Mashali na kulirudia dirisha kuangalia kilichokuwa kikiendelea kati ya mkewe, mama Muro pamoja na mama Kirumba.

* * *

Bado mama Mashali alikuwa chini akitapatapa. Pumzi zilimuishia, kijasho kikaanza kutambaa katika mwili wake kutokea shingoni.

“Mama Mashali, mama Mashali!” aliita mama Kirumba baada ya kufika eneo la tukio.

“Sasa hivi ndiyo unajifanya mama Mashali!” aliropoka mama Muro.

“Kwani nimefanyaje jamani, au nini kimetokea maana sielewi!”

“Huelewi?”

“Ndiyo sielewi!”

“Utaelewa tu sasa!”

“Lakini mama Muro, mbona unaniweka njia panda!”

“Na nitakuweka sana njia panda, mpaka ukweli utaeleweka mwaka huu!”

Maneno yale yalimuingia kichwani mama Kirumba pasipo kuyapatia jibu. Kichwani alikuwa na mambo mawili, moja kushtukiwa kuwa amemuingiza mzee Mashali chumbani kwake ama kutakuwa na mambo yao binafsi yaliyofanya kuchukiwa ghafla.

“Hizo sendozi ulizozishika za nani?”

Mama Kirumba akashtuka, akaziangalia kwa mara nyingine.

“Hizi nilizozishika?”

“Ndiyo?”

“Ahhaaa mama Muro, hizi sendozi si za mwanangu Kirumba!”

Aibu ilimtawala ghafla mama Muro baada ya kusogeza macho yake karibu na zile sendozi, kweli zilikuwa za mtoto wake wa miaka kumi na mbili.

“Basi shosti,” aliongea mama Muro kwa aibu na kushika kanga huku akishirikiana na mama Kirumba kumpepea mama Mashali.

“Habari zenu!” Sauti ya mzee Mashali ilisikika. Alikuwa ameshafika eneo lile akiwa na fuko lake lililojaa mapazia.

“Shemeji!” aliropoka mama Muro kwa aibu.

“Kafanyaje tena mwenzenu?”

“Si unajua tena shemeji sisi wanawake, tulikuwa katika mazungumzo ghafla akasema anajisikia kizunguzungu tukashangaa amelegea na kuanguka.”

Mzee Mashali alishajua presha inayomsumbua mke wake pindi akipata mshtuko wowote. Alishajua kilichomfanya kunyong’onyea na kuanguka pale kuwa ni kutokana na yeye.

“Mama Mashali?” alimwita mke wake huku akimshika mkono. Akashtuka!

“Baba Mashali?”

“Embu amka, amka!”

Mama Mashali alikubali kuamka kwa kushikwa mkono na baba Mashali. Hakuwa anaelewa chochote baada ya kuwaona mama Muro, Mama Kirumba na muwewe wakiwa pamoja. Kumbukumbu zote za tukio lililotokea muda mfupi uliopita zilikuwa zimeshakata katika akili yake.

“Haya twende nyumbani!”

Waliondoka na kumwacha mama Kirumba akibaki na mama Muro.

“Haya shemeji, tutakuja kumuona mama Mashali baadaye!”

* * *

Mama Kirumba alirudi hadi nyumbani kwake, breki ya kwanza alipitiliza hadi chumbani kwake kuyaangalia yale mapazia. Alijua fika mzee Mashali atakuwa ameyatoa kwakuwa hakuwa amemlipa hela zaidi ya kukubaliana bei itakuwa shilingi elfu themanini.

“Waoooh! Yanapendezaje!” alijiongelea mwenyewe na kujitupa kitandani.

Mawazo yakamjia, akavuta picha tukio zima lilivyotokea na kufananisha na filamu za maigizo. Hakuamini kama katika kitanda alichokuwepo alikuwa amelala na mzee Mashali na kumpa tunda.

“Lakini anauweza utundu!”

Akavuta picha zaidi na kuyafikiria maneno aliyokuwa akiambiwa na mzee Mashali wakati yupo kifuani kwake.

“Eti cheki una mapaja mazuri, cheki kifua, tumbo, duu mzee Mashali bwana!”

Alimaliza kuwaza na kushuka kitandani kisha akajiangalia umbo lake vizuri. Akahamia eneo la pembeni kisha akazungusha shingo na kujiangalia eneo la nyuma kwa jinsi lilivyoumbika.

“Na ana bahati tu nilimpa kidogo, je tungekesha?”

Mzuka ulikuwa umempanda. Akili ikamtuma moja kwa moja kuchukua simu yake na kuanza kumchokoza mzee Mashali kwa kuandika meseji.

“Nataka tena!”

Je, nini kiliendelea hapo? Usikose chombezo hili wiki ijayo.

Leave A Reply