The House of Favourite Newspapers

Mapenzi ya mdomo sawa, lakini unajua kansa ya koo?

0

f79776428c810d2e492c35bf2e5b8b37MAPENZI kwa njia ya mdomo yamekuwa yakizidi kuongezeka siku hadi siku na kwa kasi kubwa hasa miongoni mwa vijana.

Mapenzi haya au kwa lugha nyingine ngono ya kinywa (oral sex) ni ile tabia ya wahusika kunyonyana ndimi na sehemu nyingine nyeti. Wengi wanaamini ni uhodari wa kisasa wakati huu wa sayansi na teknolojia.

Lakini pamoja na wengi kuitumia njia hii kukamilisha furaha yao ya mapenzi, tabia hii huchangia wahusika kupata magonjwa mbalimbali, hususan ugonjwa mbaya wa kansa ya koo.

sexKUNDI BAYA
Wataalam kutoka nchi mbalimbali wamethibitisha kwamba kufanya mapenzi kwa njia ya mdomo husababisha uwezekano wa mhusika kupata saratani ya koo. Hii, watafiti wanasema huwatokea zaidi wanaume kuliko wanawake.

TUICHAMBUE KWANZA KANSA HII
Kansa ya koo ni aina ya mabadiliko ya seli ambazo hukua bila kudhibitiwa na mwili wenyewe. Kansa hii huathiri sehemu za mdomoni, kooni, kwenye kiboksi cha sauti (vocal cord) na katika mrija wa kupitisha chakula.

Hata hivyo, wapo wanaopata kansa hii nje ya kufanya ngono kwa njia ya kinywa, lakini uchunguzi wa kitaalam umeonesha kuwa, ngono ya mdomo huchangia kwa sehemu kubwa tatizo hili.

ATHARI NYINGINE
Pia utafiti unaonesha kuwa ngono ya mdomo inaweza kusababisha kuambukizwa kwa magonjwa ya zinaa kama vile kisonono na kaswende. Maambukizi haya hutoka sehemu za siri kwenda kwenye mdomo na kooni.

KUNA NGONO YA MDOMO ILIYO SALAMA?
Wataalam wanasema kuwa virusi vinavyosababisha maambukizi haya ni HPV (Human Papillomavirus). Kwa hiyo kama mpenzi atakuwa na virusi hivi ndipo hatari hutokea lakini kama hatakuwa na virusi hivyo, usalama upo.

Hivyo, wenye usalama wa njia hii ni wale tu wasio na mpenzi zaidi ya mmoja. Tafsiri ya hapa ni kwamba, wenye wapenzi zaidi ya mmoja wapo hatarini zaidi kupata ugonjwa huu.

USHAURI WA BURE
Ni vyema kama wapenzi watajielewa na kuachana na aina hii ya mapenzi ambayo ina hatari kubwa kiafya. Njia sahihi na ya ki-Mungu inajulikana hivyo ni vizuri watu wakasubiri mpaka ndoa ndipo waingie kwenye mapenzi ya tendo la ndoa ambayo ni halali na katika uaminifu wote.
Tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine kali zaidi.

Leave A Reply