The House of Favourite Newspapers

Marekani Imesimama, Clinton Vs Trump Kura Kupigwa Leo

trump-na-clintonMAREKANI: WAGOMBEA Urais wa Marekani, Bi. Hillary Clinton (Democratic) na Donald Trump (Trump) wamefanya mikutano ya mwisho ya kumalizia kampeni zao na kuwahimiza raia wa Marekani wawapigie kura zikiwa zimesalia saa chache kabla ya uchaguzi kufanyika.

Wote wawili wamefanya mikutano ya kampeni zao kwa kujikita zaidi katika majimbo ya kushindaniwa ya Carolina Kaskazini, Pennsylvania na Michigan.

marekaniii Bi Clinton

Bi Clinton amewahimiza wapiga kura kuunga mkono kuwepo kwa “Marekani yenye matumaini, inayojumuisha wote na yenye ukarimu”.

Bw Trump naye amewaambia wafuasi wake kwamba wana “fursa nzuri ya kuvunja mfumo mbovu na usio na maadili”.

Kura za maoni zinaonesha Bi Clinton wa Chama cha Democratic akiwa asilimia nne mbele ya mpinzani wake Bw Trump wa Chama cha Republican huku wapiga kura wengi kuliko awali, zaidi ya 46 milioni, tayari wamepiga kura za mapema.

marekanisTrump

Kuna ishara za wapiga kura wa asili ya Kihispania (Latino/Mexico) kujitoleza kwa wingi, jambo ambalo wengi wanaamini litamfaa Bi Clinton.

Uchaguzi mkuu unafanyika baada ya kampeni kali ambapo wapiga kura walirushiana matusi na kila mmoja alikabiliwa na kashfa.

Kwenye hafla Philadelphia, Pennsylvania, Bi Clinton ameungana na nyota Bruce Springsteen na Jon Bon Jovi jukwaani pamoja na mumewe Bill, Rais Obama na mkewe Michelle.

   obamaRais Obama akihutubia kwenye mkutano wa Clinton huko New Hampshire.

Rais Obama amewataka wapiga kura kukataa kutawaliwa na woga na badala yake waamue kukumbatia matumaini.

Mkutano wa mwisho wa kampeni wa Bi Clinton ulikuwa Raleigh, Carolina Kaskazini, ambao angemshirikisha mwanamuziki Lady Gaga.

Awali, alisema kwenye mahojiano redioni kwamba akishinda atampigia simu Bw Trump na kwamba anatumai mgombea huyo wa Chama cha Republican anaweza “kutekeleza mchango muhimu” katika kuunganisha tena taifa hilo.

marekani-1Mtoto wa kiume wa Trump, Eric Trump na mkewe, Lara Yunaska wakisubili kuanza kwa mkutano wa kampeni za baba yao.

Bw Trump, kwenye mkutano wake wa kampeni mjini Scranton katika jimbo hilo alisisitiza kwamba kampeni yake imekuwa ikiimarika. Mkutano wake wa mwisho aliufanyia Grand Rapids, Michigan.

Awali, aliwaambia wafuasi wake katika Jimbo la Florida kwamba yeye “si mwanasiasa” na kwamba anawajali wao pekee.

Mfanyabiashara huyo alimweleza Bi Clinton kama “mtu mwovu zaidi aliyewahi kuomba kuchagulikuwa kuwa rais”, akirejelea uchunguzi wa FBI kuhusu hatua ya Bi Clinton ya kutumia sava ya kibinafsi ya barua pepe kutuma barua pepe rasmi alipokuwa waziri wa mambo ya nje kati ya 2009 na 2013.

Jumapili, Bi Clinton alipata nafuu baada ya FBI kusema barua pepe mpya zilizokuwa zimegunduliwa kwenye uchunguzi mwingine hazikutoa ushahidi wowote wa kumpata na hatia.

Hayo yakijiri, meneja wa kampeni wa Bw Trump, Kellyanne Conway amepuuzilia mbali wasiwasi miongoni mwa jamii ya kimataifa kuhusu uwezekano wa mgombea huyo wa Republican kushinda.

marekani-2Mtoto wa Bi. Clinton, Chelsea Clinton akimnadi mama yake.

Akiongea na BBC Jumatatu, alisema ukosoaji ambao umekuwa ukitoka nje ya nchi “hauashirii sifa halisi za Donald Trump na sababu zinazomfanya awanie urais na sifa atakazokuwa nazo jukwaa la kimataifa akishinda”.

Rais wa Ufaransa Francois Hollande alikuwa amesema bilionea huyo humfanya “ahisi kutapika”.

Bw Trump amekabiliwa na shutuma kali hasa kutokana na madai ya kuwadhalilisha kingono wanawake, madai ambayo Bw Trump ameyakanusha.

marekaniAidha, kuna kadha zilizotolewa zikimuonesha akitoa matamshi ya kuwadhalilisha wanawake. Bw Trump alisema mazungumzo hayo yalikuwa ya mzaha na ya faraghani.

Bw Trump pia ametuhumiwa kwa kueneza chuki dhidi ya wageni baada ya kuapa kuwapiga marufuku Waislamu wasiingie Marekani kwa muda kama njia ya kukabiliana na ugaidi.

Aliwaeleza raia wa Maexico kuwa “wabakaji” na kadhalika, alisema angejenga ukuta kwenye mpaka wa Marekani kuwazuia Wamarekani wasiingie nchini humo.

Comments are closed.