The House of Favourite Newspapers

Marioo: Mwaka 2022 Tuzo Zitakuwa Za Kutoshaza

0

MUZIKI ni ajira, lakini pia ni biashara kubwa ndiyo maana nchini Nigeria wanaichukulia serious tofauti na
wengi wanavyoiona!

 

Kila mwaka wanazaliwa wasanii wapya ambao wanakuja kuwa wakubwa na kukimbiza ndani na nje ya nchi ndiyo maana huwezi kushangaa kuna kipindi wanaibuka hata watano au saba kwa mpigo na wote wakakubalika.

Tumeona kipindi wanaibuka Davido, Yemi Alade, Wizkid, Burna Boy na nwengine ambao leo ni
wasanii wakubwa.

 


Kibongobongo wasanii wengi
wamekuwa wakizaliwa, lakini siyo kwa kiwango cha kutoboa
kimataifa, lakini wameendelea
kudumu kwenye gemu.

 

Omary Ally Mwanga. Ndiyo! Najua utashangaa kuliona jina hilo japo mtaani huko Temeke alipokulia wanalitambua sana! Unaweza kumuita kwa jina lingine maarufu la Marioo.

 

Ni zao kutoka kwenye tasnia ya Bongo Fleva mwenye kipaji cha hali ya juu katika kuimba na kuandika mashairi.
Marioo amejizolea umaarufu
baada ya kuwatungia nyimbo wasanii wengi wakubwa kama Nampa Papa wa Gigy Money, Pambe wa Christian Bella, Nabembea wa Ditto, Bado ya Mwasiti, Sawa ya Msami na Wasikudanganye ya Nandy.

 


Wachache wanalitambua hilo
kwamba hadi wale wakongwe kuna muda wanapungukiwa busara za kuandika mashairi hivyo kuomba msaada ili kuendelea kupeta kimuziki.

 


Gazeti la IJUMAA
limefanya mahojiano ya kufunga mwaka na Marioo aliyekimbiza na ngoma kibao kama Ifunanya, Wauwe, Yale, Inatosha na Chibonge ambapo kwa sasa atamba na ngoma zake za Mama Amina, Wow na Beer Tamu;


IJUMAA:
Mambo vipi Toto Bad?

MARIOO: Salama kabisa.

IJUMAA: Hongera umetajwa kwenye listi ya vijana wa moto kwa mwaka huu unaoelekea ukingoni wa 2021.

 

MARIOO: Ahsante sana. Pia niwashukuru sana mashabiki wangu maana bila wao mimi siyo kitu.
IJUMAA:
Kwa mwaka 2021, mashabiki na baadhi ya wasanii wenzako walikusifu mno kwa kile
ambacho ulikifanya, wanasema
ulifanya mambo makubwa kwenye gemu ndani ya muda mfupi, kwa
mwaka 2022 watarajie nini?

 

MARIOO: (anacheka) nashukuru sana kwa comments (maoni) yao, nimezipokea vizuri.

 

Kikubwa ni kuzidi kujituma kwani mwaka juzi nilivyoanza muziki na Ngoma ya Dar Pagumu haikuwa kazi rahisi.
Ni kweli mwaka huu nimefanya
vizuri. Kwa hiyo niseme tu kwamba nitazidi kuchana mawimbi na ninaahidi kufanya mambo mengi makubwa kiasi cha kushangaza dunia.


IJUMAA:
Unawaambia nini mashabiki wako?

 

MARIOO: Namuomba Mungu tu anijaalie pumzi kwa sababu mwaka unaoingia WA 2022 nadhani ndiyo nitafanya muziki mzuri kuliko hata 2021.

 


IJUMAA:
Nini mipango yako au unajiona wapi baada ya mwaka huu?


MARIOO:
Malengo yangu ni kuupeleka muziki wa Bongo Fleva mbali huko duniani.

 


IJUMAA:
Unadhani utaweza kuupeleka huko unapopataka?

MARIOO: Kama ilivyo kwa wasanii wengi, na mimi natamani kufanya kolabo na wasanii wakubwa duniani, hilo najua litafanikiwa kwani plans (mipango) zipo nyingi, zikitiki tu, mashabiki watanisikia.

IJUMAA: Hivi ni kweli kwamba muziki wa sasa umeshuka?

MARIOO: Lisemwalo lipo, lakini kwa upande wangu nipo kwa ajili ya kufanya muendelezo kama Bongo
Fleva itakuwa haiendi vizuri sijui
itashuka, mimi pia nitaumia maana ninategemewa kuiinua. Kikubwa
ni kuleta sound tofautitofauti kwa
kubadilikabadilika

IJUMAA: Marioo ni miongoni mwa wasanii wanaofanya poa kwa sasa na tayari umeanza kuvuka mipaka kwani
mwaka huu ulitajwa
na waandaaji wa Tuzo za Sound City kuwa miongoni mwa wasanii wanaokuja kwa kasi barani
Afrika…

 

MARIOO: Ni kweli kabisa na nakubali.

IJUMAA: Miongoni mwa ngoma zako zilizokuweka kwenye ramani vilivyo ni Inatosha, je, mwakani tutegemee kujaza kabati la tuzo?


MARIOO:
Yaani siyo za kuulizia, zitakuwa za kutosha hadi patakosekana pa kuziweka, tuseme insha-Allah.

IJUMAA: Baadhi ya mashabiki mitandaoni wamekupa tahadhari wakisema uwe makini, usilewe sifa kwani unaweza kupotea…


MARIOO:
Ni kweli kabisa na mimi huwa napenda sana kusoma komenti za mashabiki wangu ili nijue wapi ninapokosea ili niweze kujirekebisha.


IJUMAA:
Ahsante sana kwa ushirikiano wako.

MARIOO: Nashukuru pia.

MAKALA: KHADIJA BAKARI

Leave A Reply