The House of Favourite Newspapers

Martinez, Varane Nje Msimu Mzima Manchester United

0
Lisandro Martinez ‘The Butcher’

MANCHESTER United imepata pigo baada ya nyota wake muhimu wa safu ya ulinzi, Lisandro Martinez ‘The Butcher’ na Raphael Varane kutupwa nje ya uwanja mpaka msimu ujao.

Martinez ametupwa nje ya uwanja mpaka msimu ujao baada ya kuumia kwenye mchezo wa robo fainali ya Europa League dhidi ya Sevilla, Alhamisi wiki hii.

Baada ya kufanyiwa vipimo, beki huyo imebainika amepata majeraha makubwa katika mguu wake.

The Butcher baada ya kuumia dhidi ya Sevilla, alitolewa uwanjani akiwa amebebwa.

Katika mchezo huohuo, Man United ilipata pigo lingine kwa beki wake Mfaransa, Raphael Varane ambaye naye aliumia.

Varane taarifa za awali zimeeleza atakuwa nje kwa wiki tatu, lakini huenda ikawa mpaka msimu ujao kutokana na mambo yalivyo.

Hili ni pigo kubwa kwa Man United ambao kwa sasa itawakosa mabeki hao wawili wa kati, huku staa wao Marcus Rashford haijafahamika atarejea lini uwanjani baada ya kuumia wikiendi iliyopita.

Kumbuka Man United ina kibarua kikubwa kuwania kumaliza ndani ya nne bora kwenye Premier League msimu huu.

Pia wana kibarua cha kusaka tiketi ya kwenda nusu fainali ya Europa League, wakicheza ugenini dhidi ya Sevilla, Alhamisi ijayo. Bado wana kazi mbele ya Brighton katika nusu fainali ya Kombe la FA.

MFAHAMU ASHRAF HAKIM MCHEZAJI ALIYETOKA KWENYE FAMILIYA YA KIMASIKINI NA KUISHANGAZA DUNIA…

Leave A Reply