The House of Favourite Newspapers

Masau Bwire Afunguka Kutua Simba -Video

0

WAKATI tetesi zikieleza kuwa muda wowote Masau Bwire ambaye ni Ofisa Habari wa Ruvu Shooting atakabidhiwa mikoba ya kuwa msemaji wa Simba, kiongozi huyo ameibuka na kuweka wazi suala hilo.


Kwa sasa nafasi ya usemaji
wa Simba inakaimiwa na Ezekiel Kwamwaga aliyepewa miezi miwili na alibainisha kwamba ataondoka katika nafasi hiyo muda wake ukiisha.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Bwire alisema: “Hizo za kuhusu mimi kwenda Simba ni tetesi zipo kila kona, siku ikifika watu watajua pale wenye mamlaka watakaposema.

 

“Unajua mimi ni mzalendo si kwa Simba tu hata kwa Yanga nimefanya sana kutoa hamasa hasa kwenye masuala yanayohusu taifa. Mimi nina kawaida ya kuhamasisha pale timu inapokuwa na jambo linaloihusu Tanzania kwa kuwa ninajua hiyo ni fursa.

 

“Najua haya yametokana na watu kuona mimi nikizungumzia kuhusu Simba lakini hii Simba Day kuna watu wanafuatilia nje ya Tanzania, wakiona kuna nyomi, watu wanaona kuna kitu kinaendelea, tushirikiane Watanzania tuache roho ya korosho.

 

“Kwa mfano tarehe 25/11-15/12 kutakuwa na mashindano ya soka la wenye ulemavu na Tanzania itakuwa mwenyeji, mpaka wakupe fursa hiyo ni watu wamekuamini na mimi nitakuwa msemaji rasmi kwenye mashindano hayo makubwa yatahusisha timu 16 na wanatafuta timu 8 zitakazoshiriki mashindano Uturuki, hivyo Watanzania tuungane,” alisema Bwire.


Hivi karibuni, Kamwaga aliliambia
Championi Jumamosi kuwa mchakato wa kumsaka Ofisa Habari ukikamilika kila kitu kitawekwa wazi.

STORI NA LUNYAMADZO MLYUKA

Leave A Reply