The House of Favourite Newspapers

Mashabiki wa Man Utd Waishambulia Nyumba ya Ed Woodward

0

MASHABIKI  zaidi ya 20 wa Manchester United waishambulia nyumba ya Makamu Mwenyekiti Mtendaji wa klabu hiyo, Ed Woodward huko Cheshire.

Mashabiki hao walikuwa wakiimba “atakufa”. Video iliyotumwa kwenye Mitandao ya kijamii ilionyesha mtu akitoa sauti juu ya lango kubwa, wakati wengine waliimba nyimbo zilizo mlenga Woodward mwenye umri wa miaka 48.

Makamu Mwenyekiti Mtendaji wa Manchester United, Ed Woodward.

Woodward, ambaye ameoa na ana watoto wawili wadogo, hakuwepo wakati wa maandamano hayo yaliyokuwa yakishinikiza kumtoa madarakani katika nafasi yake ndani ya Manchester United, na Taarifa ya United imesema mtu yeyote atakayebainika kufanya kosa hilo la jinai au kukutwa na hatia atazuiliwa kuingia uwanjani kwa maisha yote.

Tukio hilo linakumbusha shambulio lingine, mnamo 2004, kwenye gari la wakati huo mkurugenzi wa Klabu hiyo ni Maurice Watkins, ambaye hisa zake zilimalizika baada ya kununuliwa na Malcolm Glazer.

 

Woodward alimshauri Malcolm Glazer na familia ya Glazer kuichukua Klabu na kufanikiwa mwaka 2005 kabla ya kuajiriwa kama mfanyakazi mwandamizi.

Leave A Reply