Maski ya ndizi kwa kipindi cha upepo

bananamaskWatu wengi kwa sasa wamekuwa na ngozi mbaya, wengine wanafikia hatua ya kuchubuka ngozi sababu ikiwa ni hali ya hewa ambayo imebadilika kwa kuwepo na upepo mkali, sasa ukiona hali hii tumia maski ya ndizi ili kuilinda ngozi yako.

Mahitaji

Ndizi iliyomenywa 1

Kijiko 1 cha asali

Mafuta ya mzaituni kijiko 1

Kibakuli cha kuchanganyia

Jinsi ya kufanya

Changanya vyote kwa pamoja kisha saga kupata mchanganyiko mmoja.

Baada ya hapo, paka usoni mpaka shingoni kisha kaa kwa muda wa dakika 10.

Ukishamaliza muda huo osha uso wako, paka losheni au cream unayotumia. Tumia maski hii kwa wiki mara moja.

Faida ya maski hii

Asali inasaidia kukufanya uwe na ngozi laini inayoteleza, ndizi inasaidia kupunguza mafuta yaliyo kwenye ngozi.

Mafuta ya mzaituni yanaifanya ngozi kutokakamaa, hasa kipindi hiki cha upepo mkali.


Loading...

Toa comment