The House of Favourite Newspapers

Mastaa Simba Wawekewa Milioni 20 Mezani

0

 

Said Ally |CHAMPIONI| Dar es Salaam

BAADA ya kufanikiwa kupata pointi tatu mbele ya Mbao FC, uongozi wa timu ya Simba umeweka milioni 20 kwa ajili ya kuhakikisha kikosi hicho kinapata ushindi mbele ya Toto Africans kwenye mechi itakayopigwa Jumamosi hii.

Simba itakuwa na kibarua kingine cha kusaka pointi tatu katika Uwanja wa Kirumba mbele ya Toto ambao wamekuwa wakiwasumbua hasa wanapocheza uwanjani hapo na mara ya mwisho Simba kucheza uwanjani hapo waliambulia sare ya bao 1-1.

Mmoja wa mabosi kutoka ndani ya Simba amelieleza Championi Jumatano kuwa, fedha hizo ni zile ambazo hutolewa kwa ajili ya bonasi ya kushinda mechi ambapo wameamua kuwasubirisha fedha zao walipoifunga Mbao ambapo sasa watawapa baada ya mechi hiyo na Toto kumalizika.

“Tumetenga milioni 20 kwa ajili ya kuifunga Toto ambayo imekuwa ikitupa shida sana hasa ikicheza hapa kwao na tunaamini kwa jinsi mwenendo wetu ulivyo, ni lazima watupe tu hizo pointi watake wasitake.

“Baada ya mechi na Mbao hatukuwapa wachezaji zile fedha zao za bonasi ya kila baada ya mechi ambapo tumeziunganisha mpaka washinde mechi hii na Toto ndipo tutawapa kwa pamoja ambapo zitakuwa milioni 20,” alisema bosi huyo.

Leave A Reply