The House of Favourite Newspapers

Mastaa wa Nje Wanaogelea Noti, Wetu Hawana Habari

0
Wema Sepetu.

WAKATI michezo na sanaa imekuwa ni kazi na biashara inayowaingizia fedha nyingi watu wa mataifa ya nje kwa miaka mingi, kwa muda mrefu, Watanzania wameifanya kama sehemu ya kupata umaarufu na sifa. Si soka, maigizo, vichekesho, filamu wala muziki, wengi wameifanya kimazoea hadi kiasi cha muongo mmoja na ushee uliopita, watu walipoanza kushtuka na kuona kumbe unaweza kucheza mchezo uupendao, lakini ikawa ni kazi ya mamilioni ya fedha.

Omotola Jalade Ekeinde

Kuanzia wanasoka wa umaarufu kama akina Jella Mtagwa hadi kizazi kilichoshtuka cha kina Juma Kaseja, wachekeshaji wa mitaani mpaka wanapoibuka akina MC Pilipili, filamu enzi za Fimbo ya Mnyonge (Yomba Yomba) hadi Bongo Movie na muziki wa bendi hadi Bongo Fleva.

Jacqueline Wolper.

Akina Mtagwa walicheza kupata sifa na umaarufu, lakini hawakulipwa fedha na hata picha zake zilipotumika katika stempu, kwake ilikuwa ni ufahari pasipo kujua alipaswa kuvuna mamilioni. Lakini vijana wa sasa, ambao hawafikii hata robo ya umahiri wa kizazi chao, wanasajiliwa kwa fedha nyingi na kulipwa mishahara minono!

 

Vivyo hivyo, wachekeshaji wenye vipaji kama akina Mzee Small, wamekufa masikini wakati vijana hawa wa sasa, wanapiga fedha nyingi wakiwa hawafikii hata kidogo umahiri wa kizazi cha akina Small, King Majuto, Mzee Jangala, Onyango na wenzao wa namna hiyo. Huku kwenye muziki nako mambo ndiyo yanatia simanzi.

Mercy Johnson.

Achana na waasisi wa muziki wa kizazi kipya ambao waliufanya kwa nguvu na kulilia malipo lakini wakipatakebehi kutoka kwa wadau, nawazungumzia wazee wangu wa hizi bendi kongwe, twende pale Msondo, tuje huku Sikinde, kabla ya kuelekea kwa African Stars na FM Academia. Ni kwa misingi hii, ninashangazwa na dada zangu wa Bongo Movie.

 

Nilikuwa napitia majarida na mitandao ili kuona hali za maisha ya waigizaji wa kike wa Nigeria, ndipo kwa uchungu, nikawakumbuka dada zangu. Wapo katika kipindi ambacho filamu zinauza na watu wanaendesha na kupata mafanikio kupitia sanaa hiyo. Lakini ukiwatazama, hawaonekani kuitumia vizuri sanaa yao hiyo. Kule Nigeria, waigizaji wa kike siyo watu ambao wanaingilika kirahisi katika ushawishi wa kimapenzi kama inavyotokea hapa nyumbani.

 

Wakiingia katika uhusiano wa kimapenzi ni kwa sababu ya kibinadamu tu, si kimasilahi kama unavyoweza kuwatafsiri mastaa wa nyumbani. Rita Dominic, yule muigizaji ambaye wakati mwingine hu-ekti kama changudoa, mapepe na asiye mtulivu, lakini pia akichezanafasi za umakini ni balaa, ni staa mwenye mkwanja mrefu kuliko waigizaji wote wa kike kule Nollywood, ambao ni kiasi cha Naira (fedha za huko) milioni 950, ambazo ukizibadili kwa madafu ni kama bilioni tatu na ushee.

 

Achana na Rita, njoo kwa Genevieve Nnaji, mkali mwingine wa kike mwenye mkwanja wa haja kule Nigeria. Yeye anaogelea kwenye dimbwi lenye fedha kiasi cha Naira milioni 850. Licha ya kuwa staa mkubwa na miongoni mwa waigizaji mwenye mashabiki wengi, pia ni mwekezaji mkubwa kati ya wasanii wenye heshima.

 

Haya, mwangalie Omotola Ekeyinde, yule muigizaji ambaye staa wetu Wema Sepetu alimleta hapa kwa ajili ya uzinduzi wa filamu yake. Yule mdada, si wa mchezomchezo, akaunti yake inasoma kiasi cha Naira milioni 550 ambazo kibongobongo ni kama bilioni moja na kitu.

 

Siyo hao tu, lakini ukisikia majina ya waigizaji kama Mercy Johnson, Ini Edo, Funke Akindele nao wote wana fedha ambazo zinawafanya wawe levo flan ambazo mtu wa vihela vyake vya dili, hawezi kumchezea. Ni vigumu kuhukumu kuwa waigizaji wetu hawana kitu, lakini aina ya maisha wanayoenda nayo, ni rahisi kutabiri.

 

Ni kweli, karibu kila mmoja ana kampuni yake ya mambo ya entertainments, Wema Sepetu anayo, Kajala pia, Johari naye, Odama na wengine wana miradi wanaendesha kama maduka ya nguo, vipodozi na baadhi yao maduka ya vinywaji.

 

Hata hivyo, biashara zao haziko kama ambavyo wangestahili kuwa kwa kutumia umaarufu wao kupitia filamu. Watu wanapenda filamu na wao tayari wamelishika soko, lakini wanashindwa kulitumia, badala yake bado wanategemea ‘wadosi’ ndiyo.

 

Leave A Reply