The House of Favourite Newspapers

Mastaa wa Soka, Bongo Movie Waifungukia Sokabet

0
Viongozi wa Sokabet wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wachezaji wa Majimaji.

KAMPUNI ya Mchezo wa Kubahatisha ya Sokabet, jana Jumatatu ilifanya uzinduzi wake rasmi katika Hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam ambapo mastaa mbalimbali wa soka na tasnia ya filamu nchini walihudhuria uzinduzi huo.

Mchezaji wa zamani wa Yanga na Timu ya Taifa, Taifa Stars, Edibily Jonas Lunyamila akishuhudia uzinduzi huo.

Miongoni mwa mastaa hao ni pamoja na mwigizaji na mchekeshaji maarufu hapa nchini, Mboto Haji na wanasoka wa zamani kama Ally Mayay, Manyika Peter Manyika, Boniface Pawasa, Edibily Lunyamila na wengineo.

Mbali na uzinduzi huo, pia Sokabet iliingia mkataba wa udhamini wa mwaka mmoja na timu ya Majimaji FC ya Songea wenye thamani ya Sh milioni 150.

Wachezaji wa zamani, kutoka kushoto ni  Aaron Nyanda, Boniface Pawasa, Ally Mayay na Manyika Peter Manyika.

Akizungumzia tukio hilo, Mayay alisema: “Ni kitu cha faraja kuona Sokabet imeanzishwa hapa nchini kwani ukiangalia fedha inapatikana katika mpira wa miguu na inarudi katika kuendeleza mchezo wa soka kutokana na udhamini huu kwa Majimaji.

Mratibu wa Sokabet, Ruhinda akimkabidhi jezi yenye nembo ya Sokabet mchezaji wa Majimaji, Jerryson Tegete.

“Sokabet pamoja na kufanya biashara, lakini pia inachangia kusaidia mchezo wa soka kukua kwani udhamini huu unawafanya Majimaji kuwa na uwezo wa kujikimu katika masuala ya usafiri, malazi na mengineyo, walichokifanya Sokabet ni kitu cha kuungwa mkono.”

 

Manyika Peter Manyika akifungukia Sokabet.

Naye Manyika, alikuwa na haya ya kusema: “Najisikia faraja kuwepo katika uzinduzi huu na nashukuru Kampuni ya Sokabet kutukumbuka watu kama sisi ambao tuliwahi kucheza soka siku za nyuma.

 

Mboto akiifungukia Sokabet.

“Nilichokiona kwenye Sokabet ambacho ni tofauti na kwingine, ni jinsi wanavyoweza kukupa salio unapojiunga nao, ukiangalia kampuni zingine za kubeti hakuna kitu kama hicho. Sokabeti wamekuja tofauti na wamekuja kwa ajili ya kuwasaidia watu wengi, mashabiki waiunge mkono Sokabet kwani imekuja kwa ajili yao.”

Mboto akifuatilia uzinduzi huo.

Kwa upande wa Mboto, naye alisema: “Tumeona makampuni mengi yakijitoa katika kuwekeza sehemu mbalimbali, hivyo basi walichokifanya Sokabet nacho ni cha kiungwana, kwanza kuwaletea Watanzania unafuu wa kubeti, lakini pia udhamini wao kwa Majimaji.

“Binafsi inapocheza Yanga huwa nabeti kwamba inashinda, na inapocheza Simba nabeti inafungwa. Kwa hapa Sokabet wanarahisisha mambo kwani ukishinda tu mkwanja wako fasta unaingia katika simu bila ya longolongo.”

Ili uweze kubeti na SOKABET ingia katika tovuti ya www.sokabet.co.tz

Namba yako ya ushindi ni 335757

 

Kumbuka kuwa ili kujiunga na kubashiri ili kuvuna fedha unatakiwa kutembelea tovuti ya www.sokabet.co.tz ambapo humo ndani una nafasi ya kushinda hadi shilingi milioni 100 kwa kuweka Sh 1,000 tu.

SHUHUDIA UZINDUZI HUO.

 

Leave A Reply