The House of Favourite Newspapers

Mgombea wa upinzani aongoza katika uchaguzi wa rais nchini Senegal

0
Mgombea wa upinzani nchini Senegal, Bassirou Diomaye Faye, akipiga kura katika kituo cha Ndiaganiao huko Mbour, Machi 24, 2024.

Hesabu za kwanza katika vituo vya kupigia kura katika uchaguzi wa rais uliocheleweshwa nchini Senegal Jumapili zinaonyesha mgombea wa upinzani Bassirou Diomaye Faye akiongoza.

Wafuasi wake walianza kusherekea mitaani baada ya siku ya amani ya uchaguzi ambayo wengi wanatumaini utaleta mabadiliko.

Mamilioni ya watu walijitokeza kumchagua rais wa tano wa Senegal kufuatia miaka mitatu ya msukosuko wa kisiasa ambao haujawahi kushuhudiwa na ambao ulichochea maandamano mabaya dhidi ya serikali na kuhimiza uungwaji mkono kwa upinzani.

Wapiga kura walitakiwa kumchagua mmoja kati ya wagombea 19 kuchukua nafasi ya Rais Macky Sall, ambaye anaachia ngazi baada ya muhula wa pili uliokumbwa na machafuko kutokana na kumfungulia mashtaka kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko na hofu kwamba Sall alikuwa na lengo la kurefusha muhula wake baada ya kikomo cha mihula kilichowekwa ndani ya katiba.

Rais aliye madarakani hakuwa kwenye orodha ya wagombea kwa mara ya kwanza katika historia ya Senegal.

Muungano wa vyama vinavyotawala ulimteua waziri mkuu wa zamani Amadou Ba, mwenye umri wa miaka 62 kama mgombea wake.

Hesabu za kwanza za kura zilizotangazwa kwenye televisheni zinaonyesha Faye atapata wingi wa kura, na kuchochea sherehe kubwa mitaani miongoni mwa wafuasi wa upinzani katika mji mkuu wa Dakar.

Matokeo ya mwisho yanatarajiwa Jumanne. Duru ya pili ya uchaguzi itafanyika ikiwa hakuna mgombea atakayepata zaidi ya asilimia 50 ya kura zinazohitajika ili kuepuka marudio ya uchaguzi.

Gazeti lako bora la Championi linalotoka mtaani mara mbili kwa wiki, Jumatatu na Ijumaa, sasa limekuja kivingine.
Tunatoa zawadi kwako ewe msomaji ambapo kwa kununua GAZETI LA CHAMPIONI, utapata fursa ya kuzawadiwa jezi mpya ya Simba au Yanga za msimu wa 2023/2024, pindi ununuapo gazeti letu kupitia Global App.
Soma Gazeti la Championi kwa urahisi mtandaoni kupitia Global App: https://globalapp.co.tz

Leave A Reply