The House of Favourite Newspapers

Matukio 3 Baada ya Country Wizzy Kuondoka Konde Gang

0

Baada ya kutangazwa kuondoka kwa msanii County Wizzy katika Lebo ya muziki Konde Gang World Wide kumekua na mambo mengi sana ambayo yameajitokeza, hivyo basi katika makala hii tutaangalia mambo makuu matatu ambayo yamejitokeza baada ya kuondoka kwa County Wizzy a. k. a County Boy.

Mkataba Wa Amani Kati Ya Country Wizzy Na Konde Gang

Kama tunavyofahamu wasanii wengi ambao wanakua chini ya lebo fulani maarufu, pindi wanapotaka kuondoka kunakua na mvutano baina ya pande zote mbili na kuwekea vikwanzo tofauti tofauti. Mfano mzuri ni kuondoka kwa Harmonize WCB, kuondoka kwa Rich Mavoko WCB, kuondoka kwa Killy na Cheed Kings Music na wengine wengi.

 

Lakini kwa upande wa County Wizzy ilikua tofauti kidogo ambapo mnamo siku ya tarehe 8 January 2022, Lebo ya muziki Konde Gang World Wide kupitia ukurasa wake wa Instagram ilitoa tamko juu ya kumuaga msanii huyo na kusema kwamba pande zote mbili zimelizia maelewano hayo.

Konde Gang walisema ” Taarifa, mkataba kati ya Konde Music World Wide na Country Wizzy umemalizika leo tarehe 8 January 2022. Kwaiyo kuanzia leo Country Boy atakua msanii anayejitegemea baada ya kufikia makubaliano ya pande zote mbili”.

 

Kufanyika Kwa Sherehe Ya Kumuaga Wizzy

Mbali na mkataba wa amani walioufanya kati ya Konde Music World Wide na msanii Country Wizzy, pia waliibuka na kufanya pati ya pamoja usiku wa tarehe 9 January 2022 kuamkia tarehe 10.

Hiki pia sio kitu cha kawaida kwani mtu anapoondoka lazima migogoro iwepo sasa mpaka kufikia kufanya tafrija ya pamoja, basi inaonyesha waziwazi kuwa Country Wizzy na team nzima ya Konde Music World Wide inayoongozwa na msanii Harmonize, usiku huo walisherehekea pamoja kama team ilivyokuwa awali.

 

Mfanano Wa Mawazo Kati Ya Harmonize Na Country Wizzy

Katika maagano hayo Harmonize alitumia ukurasa wake wa Instagram katika insta story yake alimuaga msanii huyo kwa kusema kuwa ” Asante kwa kuwakilisha Gang kubwa kwa miaka miwili, nakupenda sana kaka na nakutakia kila la kheri katika maisha yako mapya. Nenda kafanye vizuri nijivunie uwepo wako tupo pamoja, nyota yako ikang’ ae Rasta”.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram katika insta story yake Country Wizzy na yeye ameposti maneno ambayo aliambwa na Harmonize, hii inaonyesha jinsi gani wawili hawa bado wapo pamoja na wanaendelea kupedana.

Leave A Reply