The House of Favourite Newspapers

Mavugo: Yanga wasitukatishe tamaa, ubingwa bado wetu…

STORI: Wilbert Molandi, Dar na Derrick Lwasye, Songea | CHAMPIONI

MSHAMBULIAJI wa Simba, Mrundi, Laudit Mavugo, amewapa matumaini mashabiki wa timu hiyo kwa kuwaambia ni mapema kukata tamaa ya ubingwa wa Ligi Kuu Bara na kwamba bado wana nafasi ya kulichukua taji hilo.

Mavugo ambaye juzi alifunga bao lake la kwanza la ligi kuu tangu mzunguko wa pili uanze Desemba 17, mwaka jana, amedai baada ya kuifunga Majimaji mabao 3-0 ugenini kwenye Uwanja wa Majimaji, Songea nafasi yao ya ubingwa ni kubwa.

Simba hivi sasa ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 48 nyuma ya Yanga wenye pointi 49 kwenye msimamo wa ligi kuu.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Mavugo alisema bado mechi nyingi zimebaki kwao na watani wao Yanga, hivyo haoni sababu ya kukata tamaa ya kulichukua taji hilo.

Mavugo alisema, kikubwa wanachotakiwa ni kupambana ndani ya uwanja ili wapate matokeo mazuri kwa ajili ya kujiwekea mazingira ya kuchukua ubingwa huo.

Aliongeza kuwa, pointi moja wanayoiongoza Yanga ni ndogo ambayo anaamini kama watapambana, basi watawatoa kileleni.

“Matokeo ya mechi na Azam FC yaliwakatisha tamaa sana mashabiki kuchukua ubingwa wa ligi kuu, ni matokeo ambayo yalitusababishia tutoke kileleni katika msimamo na kuwapisha Yanga juu.

“Hivyo, hawatakiwi kukata tamaa, ninaamini kuwa bado Simba ina nafasi kubwa ya kuchukua ubingwa huo, licha ya Yanga kukaa kileleni.

“Mechi nyingi zimebaki kwetu na Yanga, hivyo hawatakiwi kukata tamaa, sisi kama wachezaji tumepanga kupambana uwanjani ili kuhakikisha tunarejea kileleni katika nafasi yetu,” alisema Mavugo.

Tucheki kupitia;

Facebook @Globalpublishers

Twitter @GlobalHabari

Instagram @GlobalPublishers

YouTube @GlobalTVTZ

Save

Save

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam

Comments are closed.