The House of Favourite Newspapers

Mayele, Aziz KI Waweka Rekodi Za Kufunga Hat Trick Yanga

0
Fiston Mayele

MASTAA wawili ndani ya Yanga, Fiston Mayele na Aziz KI, wameweka rekodi zao kuwa nyota waliofunga hat trick ndani ya kikosi hicho.

Mayele ambaye ni kinara kwa utupiaji akiwa na mabao 16 katika Ligi Kuu Bara, ana hat trick moja ambayo alifunga kwenye mchezo dhidi ya Singida Big Stars ikiwa ni ya kwanza kwa msimu wa 2022/23.

Katika ushindi wa mabao 4-1, Mayele alihusika kwenye mabao yote ambapo alifunga matatu na alitoa pasi moja ya bao.

Aziz KI mwenye mabao 9 ni wa pili kwenye kufunga hat trick ndani ya kikosi cha Yanga kwenye mechi za ligi ambapo alifunga kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar.

Katika mchezo huo, ubao wa Uwanja wa Azam Complex ulisoma Yanga 5-0 Kagera Sugar, huku Aziz Ki akihusika kwenye mabao manne, alifunga matatu na kutoa pasi moja ya bao.

Aziz KI kasepa na tuzo ya mchezaji bora ndani ya mwezi Aprili ambapo alitumia jumla ya dakika 135 kwenye mechi mbili, aliwashinda Ayoub Lyanga wa Azam FC na Jean Baleke wa Simba.

STORI NA LUNYAMADZO MLYUKA

CARINA ALIA kwa MAUMIVU! HAJA KUBWA INAVUJA KAMA MAJI TUMBONI, UTUMBO ASILIMIA 50 UMEHARIBIKA…

Leave A Reply