The House of Favourite Newspapers

Mayele, Fei Toto Wawatisha Biashara United

0

MASTAA wa Yanga wameweka wazi kuwa watakachowafanyia Biashara United ni kuchukua pointi zao tatu kwa ajili ya kujiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa msimu huu.


Yanga kwa sasa ndio
vinara wa Ligi Kuu Bara wakiwa wamejikusanyia jumla ya alama 23 mara baada ya kushinda michezo saba na kutoa sare miwili katika michezo tisa ambayo wamecheza mpaka sasa.

 

Yanga leo Jumapili Desemba 26, wanatarajiwa kumenyana na Biashara United katika mchezo unaotarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.


Akizungumza na
Championi Jumamosi, straika wa kikosi hicho, Fiston Mayele alisema kuwa ushindi ambao waliupata dhidi ya Tanzania Prisons unawafanya kupata morali ya kuendelea kupata ushindi katika mchezo wao dhidi ya Biashara huku akiweka wazi kuwa malengo yao msimu huu ni kuhakikisha
wanatwaa ubingwa wa ligi
hiyo.


“Ushindi uliopita
ugenini dhidi ya Prisons ulikuwa muhimu kwetu na utatusaidia kupata morali ya kuweza kupata matokeo katika mchezo wetu unaofuata dhidi ya Biashara United.


“Malengo yetu ni yaleyale
ubingwa msimu huu, kwa sisi wachezaji wageni tunafahamu kabla hata ya kuanza kucheza kuwa malengo msimu huu ni ubingwa, ndio maana kila mchezo kwetu tunauangalia kwa
umakini kwa ajili ya kukusanya
pointi nyingi zaidi.”

 

Naye kiungo wa timu hiyo, Feisal Salum ‘Fei Toto’, alisema: “Matokeo ya ushindi katikamchezo dhidi ya Biashara United ni ya muhimu kwetu, ili tuweze kutimiza malengo yetu, tunahitaji kushinda sana zaidi ya wapinzani wetu hivyo tutapigania ushindi ili kuweza kufikia malengo yetumsimu huu.”

Leave A Reply